Pia Miss Mbeya akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Michezo mbalimbali na watoto wa Amani.
Mlimbwende (miss) Mbeya 2016 Eunice Robert amewatembelea watoto yatima katika kituo cha Amani Nsalaga Uyole mkoani Mbeya hivi kalibuni na kuchangia baadhi ya mahitaji katika kituo hicho ikiwemo mchele, unga, sabuni, mafuta yakupikia, nguo, Daftari, Kalamu na Mafuta yakupaka. Aidha Mlimbwende huyo kutoka chuo kikuu cha Teofilo Kisanji ambaye ndiye anayeshikiria Taji la Umiss kwa sasa kwa Mkoa wa Mbeya amewaomba watu Binafsi, Mashirika ya Kidini, na Viongozi Mbalimbali wawe na mazoea ya kuwatembelea watoto yatima, Wazee, Watu wasio jiweza, Wagonjwa na wale waliopo katika Mazingira magumu na kuwasaidia kwa kuwa Jamii hiyo inahitaji Msaada kwa kiasi kikubwa hivyo sote tuguswe na hili.

No comments:
Post a Comment