jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

BENKI YA AFRIKA (BOA) KUZINDUA MATAWI ZAIDI NCHINI HIVI KARIBUINI

Share This

BENKI ya Afrika (BOA) imesema kuwa itafungua matawi yake matatu nchini mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni sehemu ya harakati zake za kuwafikia wateja wengi kwa urahisi.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa BOA, Balozi Mwanaidi Maajar, alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye hafla maalum ya kuwatakia heri ya Eid wateja wake iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, Balozi Mwanaidi alisema kuwa lengo kuu la kufungua matawi hayo ni kuhakikisha kuwa benki hiyo inakuwa mfano wa kuigwa katika kufikisha huduma zake jirani na wateja.

Alisema ni ukweli usipingika kwamba BOA imekuwa ikijitahidi na kupiga hatua katika kutekeleza majukumu mbalimbali yahusuyo fedha ili kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Balozi Mwanaidi alitaja matawi hayo kuwa ni mojawapo ni Mwenge, Mbezi Luois na Babati ambapo iwapo yakifunguliwa rasmi, benki hiyo itakuwa na jumla ya matawi 27 nchini.

Alisema imefika wakati sasa kwa wateja wa benki hiyo na watu ambao wanaohitaji kujiunga na BOA, kujitokeza katika kuchukua mikopo ili iweze kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao na hatimaye kuinua kipato chao na cha taifa kwa ujumla.

Akizungumzia hafla hiyo fupi , Balozi Mwanaidi alisema ni jambo jema katika kipindi kama hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani watu kutoa kilichozidi kama ambavyo Mungu alivyoagiza.

Alisema ni jambo la busara na lenye tija kubwa watu pindi wanapokaa na kula pamoja katika kufurahia ibada ya mwenyezi mungu.

“Huu ni utamaduni wetu hasa inapofikia kipindi kama hichi cha mwezi Ramadhani, daima tutaendelea kudumisha utamaduni huu kwa miaka ijayo kwa lengo la kuongeza upendo na mshikamano,”alisema.

Aliwashauri wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiunga na huduma zinazotolewa na benki hiyo ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia katika kuhakikisha kuwa wanakabiliana na changamoto ya ugumu wa maisha.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad