Shirika lilijinyakulia tuzo hiyo kwa kuzingatia viwango vya juu vya teknolojia na maendeleo ya burudani inayotolewa ndani ya ndege (E-BOX) pamoja na mtandao wa mawasiliano (IFEC) zinazopatikana kwenye safari zake za kimataifa. Tuzo hii ni muedelezo wa tuzo ambazo shirika limekuwa linajinyakulia kwa mwaka uliopitia kupitia huduma zake bora za ndani ya ndege zikiwemo, tuzo ya shirika bora la ndege mwaka 2015 kutoka jarida la Inflight, tuzo ya uzinduzi bora mpya kwa shirika la ndege mwaka 2016 kutoka jarida la kimataifa la PAX kwa kanda ya mashariki ya kati, pamoja na tuzo ya shirika lenye huduma bora za burudani ndani ya ndege kutoka jarida la World Travel.
Shane O'Hare, Makamu wa Rais kitengo cha Masoko wa Shirika la ndege Etihad, alisema: " Tuzo hii, iliyopigiwa kura na wasomaji wa jarida la kimataifa la PAX kwa kipindi cha miezi sita, ni utambuzi tosha juu ya dhamira ya shirika la ndege Etihad kuhakikisha wageni wetu wanaendelea kufurahia burudani bora ndani ya ndege pamoja na mtandao thabiti wa mawasiliano ndani ya ndege zetu.”
Shirika la ndege Ethihad linamiliki idadi kubwa ya ndege aina ya Airbus za kisasa pamoja na Boeing kubwa za kubeba abiria/mizigo kwa wingi na ndogo ze abiria/mizigo kidogo.
Huduma ya Tv zenye kurusha matangazo na vipindi moja kwa moja hupatikana kwenye ndege kubwa za Shirika la ndege, hii ni kuleta vipindi bora kutoka vituo saba ikiwa ni pamoja na BBC World News, Sport 24 na CNN, zikiwa zinaongoza kwa utazamajia, na CNBC, euronews , Japan NHK World Premium na Sky News Arabia.
Shirika limetambulisha huduma mpya ya burudani ndani ya ndege ya E-BOX kwa ajili ya burudani binafsi kwa kutumia mfumo wa Panasonic eX3, na ndio shirika la kwanza kufunga huduma hiyo kwenye ndege aina ya Airbus A380. Ndege zote aina ya Airbus A380s na Boeing 787s zitakuwa zimeunganishwa na mfumo huo wa burudani na vifaa vya Panasonic eX3. Mfumo huu hutoa mamia ya masaa ya burudani ya kutazamwa yenye muonekano mzuri, kwenye TV zenye ukubwa wa kuanzia inchi 11.1 kwa daraja la Uchumi, Inchi 18 kwa daraja la Biashara, Inchi 24 kwa daraja la Kwanza na Inci 32 kwa wanaotumia huduma ya “Makazi”.
Huduma nyingine za burudani ni pamoja na kuimarishwa kwa ubora wa video, kuimarishwa kwa kioo cha kugusa cha TV, uwezo wa kufanya manunuzi kwenye TV pamoja na michezo ya video, huduma ya ramani na Graphical User Interface (GUI) kwa ajili ya abiria wenye umri mdogo.
Shirika la ndege Etihad linaendelea kuleta bidhaa mpya zenye ubunifu ili kufikia malengo yake ya kubadilisha sekta ya usafiri wa anga. Tayari shirika linatoa huduma ya “Makazi” kwenye ndege zake aina ya Airbus A380, ina wahudumu binafsi waliobobea na kupata mafunzo kutoka hoteli ya Savoy yenye sifa kubwa Jijini London, wapishi wakuu kwenye daraja la Kwanza, mameneja wa vyakula na vinywaji kwenye daraja la Biashara, na wahudumu wa watoto waliohitimu kutoka chuo cha mfunzo cha Norland. Mkusanyika wa kumbi za mapumziko zinapatikana dunia nzima zikitoa huduma na vyakula kama vinavyopatikana kwenye hoteli kubwa duniani. Uwekezaji wa shirika la ndege Etihad kwenye burudani na mtandao wa mawasiliano kwenye ndege ni sehemu kubwa ya mipango yao katika kufikia mainduzi katika sekta ya usafiri wa anga.
No comments:
Post a Comment