MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva ni mfano wa kuigwa na jamii kwani ni kiongozi wa mtaa ambaye amesaidia jamii yake kwa kadiri ya uwezo wake.
Mwenyekiti huyo ambaye ameweza kusaidia vijana katika mtaa wake leo amewakabidhi pikipiki aina ya boxer vijana wa kikundi cha Polisi jamii katika mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva amesema kuwa katika kutekeleza maagizo ya Serikali kuu ya kuimalisha ulinzi na usalama wa mitaa kupitia vikundi vya Polisi jamii.
Ameyasema hayo mara baada ya kuwakabidhi Pikipiki aina ya Boxer wanakikundi cha Polisi jamii cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuimarisha ulinzi wa maeneo yote ya mtaa huo.
Lubuva ameishukuru serikali kwa kumuunga mkono katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa Serikali za Mtaa.
Pia Lubuva amewaomba wananchi wa maeneo hayo pamoja na makampuni mbalimbali taasisi mbalimbali za eneo hilo kuweza kusaidia vijana wa polisi jamii ili nao waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi jamii cha Guard, Moksin Mwalimu pikipiki ya wanakikundi cha Polisi jamii kwaajili ya kuwasaidia katika kazi yao ya ulizi hasa wakati wa usiku.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akizunumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki aina ya Boxer kwa wanakikundi cha polisi jamii cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa pikipiki hiyo ni ya mwanzo kwaajili ya kuwasaidia vijana wanaojitolea kulinda usalama wa mtaa huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akimkabidhi ufunguo wa pikipiki ambayo ni msaada mkubwa kwao kwaajili ya ulizi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi jamii cha Guard, Moksin Mwalimu akipanda pikipiki kwaajili ya kuijaribu mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment