JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAIMU KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI ATEMBELEA VITUO VYA MIPAKANI MKOANI KAGERA.

Share This
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Victoria Lembeli (katikati) akiwa pamoja na Maafisa wa Uhamiaji alipotembelea kituo kipya cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani (One Stop Border Post) katika eneo la Rusumo wilayani Ngara. Kituo hicho kilizinduliwa rasmi hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Victoria Lembeli (Katikati) akikagua mazingira katika eneo la mpaka wa Tanzania na Uganda katika eneo la Murongo wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Victoria Lembeli (Katikati) akifurahia jambo alipokuwa anakagua kituo kipya cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani (One Stop Border Post) katika eneo Kabanga, mpakani mwa Burundi na Tanzania. Kituo hicho kinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.


KAIMU Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Victoria Lembeli ametembelea vituo vya Rusumo, Kabanga, Murongo, Bugango na Mutukula. Akiwa katika vituo hivyo, Kaimu Kamishna Jenerali aliongea na maafisa Uhamiaji ikiwa pamoja na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakaabili Askari wa Uhamiaji wanaofanya kazi maeneo ya mipakani.

Kaimu Kamishna Jenerali Victoria Lembeli alisema kuwa jukumu kubwa la Idara ya Uhamiaji ni kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kutekeleza majukumu yao ya msingi baada ya kuwepo vituo vya pamoja vya mipakani (OSBP) kwani vimerahisisha utendaji ukilinganisha na siku za nyuma.

Aidha, Kaimu Kamishna Jenerali Lembeli alisema kuwa siku za nyuma wateja wa huduma za Kiuhamiaji walilazimika kupanga mistari wakiwa nchini Rwanda ili kusubiri kugongewa mihuri ya kuwaruhusu watoke halafu wakimaliza wanatembea umbali wa  zaidi ya kilometa tano ili waingie Tanzania wagongewe tena mihuri ambako pia  wanakutana na mistari mirefu jambo lilikuwa likisababisha wapoteze muda mwingi mpakani na kukata taama kwani wanakuwa wametoka safari ndefu na wamechoka.

“Baada ya vituo hivi kujengwa maafisa wa nchi zote wapo pamoja, mteja akifika anapata huduma kwa haraka na kwa wakati mmoja kwahiyo hata muda uliokuwa ukitumika umepungua angalau hata nusu, pia kutakuwepo na uwazi katika utendaji kazi wa maafisa  wetu wa pande zote mbili kwani hilo husaidia mambo kwenda vizuri zaidi” alieleza Lembeli.

Aidha alisema Idara ya Uhamiaji inalojukumu kubwa kuwawezesha wananchi kufanya biashara zao kwa urahisi kwa kuwapatia huduma zilizo bora kutokana na uboreshwaji  wa miundombinu unaoendelea kufanyika katika mipaka ya nchi yetu ili waweze kufikia malengo yao na kuona manufaa ya kuwepo kwa vituo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad