Na Mwandishi Wetu.
MABONDIA kupima uzito katika viwanja vya Mango Garden jumamosi ya Machhi 26 kwaajili ya kucheza mchezo wao Jumapili ya Machi 27 mwaka huuu ikiwa wanaendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Pasaka ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
akizungumzia mpambano uho mratibu wa pambano hilo Rajabu Mahamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayali kwa kuwa wapo na afya tele na wanaendelea na mazoezi yao ya mwisho mwisho kila mmoja akijitamba kumsambalatisha mwenzake.
Ambapo mabondia mahasimu Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ue wa vmwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe.
Mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi ambao wametasfutana kwa mda mrefu na sasa watmaliza ubishi siku ya jumapili hii.
Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote wataspima uzito siku ya jumamosi pale katika ukumbi wa Mango Garden na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka Matrch 27 uwanja wa ndani wa Taifa
'Super D' amesema mbali ya mipambano hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuku kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka mingine bondia.
Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla.
Katika mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu.



No comments:
Post a Comment