Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini
linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Wasanii Singo Mtambalike (Rich Rich) na
Elizabeth Michael (Lulu) kwa kushinda tuzo za African Magic Viewers’ Choice
Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria na kushuhudiwa
na Dunia kupitia luninga na mitandao ya kijamii.
Katika
tuzo hizo Msanii Singo Mtambalike ameshinda tuzo ya Filamu Bora ya Lugha ya
Asili (Best Local
Language - Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’ huku Msanii
Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki
(Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’
Kuteuliwa
na kushinda kwa Wasanii wa Tanzania katika tuzo hizi zilizoshirikisha wasanii na
filamu nyingi za Afrika ni ishara kwamba wasanii wetu wanakubalika, kutambuliwa
na kuthaminiwa ndani na nje ya Tanzania.
Aidha,
ushindi huu unazidi kulipa heshima na kulitangaza taifa letu katika nyanja
mbalimbali hivyo kuzidi kulifanya ling’ae na kuwa kinara katika ukanda huu wa
Afrika Mashariki na Kati.
Baraza
linatoa wito kwa wasanii na wadau wote kuzidisha ubunifu, bidii na weledi
katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo
na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kulitangaza taifa na kukuza
soko la kazi zao kimataifa.
Ni
matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata
sheria, kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi,
tuipende na kuithamini
Godfrey
Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI
No comments:
Post a Comment