Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (wa kwanza kushoto)
akitoa maelekezo kwa Kijana Frank Rowland ( katikati) kabla ya kumkabidhi banda la kuku la kisasa na
kuku 100 wa kienyeji kutoka Airtel kupitia mpango wake wa Airtel
FURSA wa kuwezesha vijana hapa nchini katika
hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao, wilaya ya Hanang, Manyara hapo jana. Wanaoshuhudia
ni ndugu zake Frank na wafanyakazi wa Airtel waliojumuika katika hafla hiyo.
Kijana Frank Rowland (wa pili kushoto) anayejishughulisha na ufugaji wa
kuku , akitoa maelekezo kwa Afisa uhusiano
na matuki wa Airtel Dangio Kaniki ( wa pili kulia) na Meneja wa mauzo kanda ya
Manyara Peter Kimaro (kushoto) jinsi anavyotunza kuku baada ya kukabidhiwa na
Airtel Tanzania, msaada wa banda la kuku
la kisasa na kuku 100 wa kienyeji ,
kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani
kwao, wilaya ya Hanang, Manyara hapo jana. Akishuhudiwa na mama yake Doris Kombe
(kulia)
Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel , Dangio Kaniki (wa pili kulia) akipiga makofi
pamoja na mama yake na Kijana aliyewezeshwa na Airtel Fursa Doris Kombe (kushoto) na wafanyakazi wengine
wa Airtel wakati wa hafla ya kumkabidhi vifaa hivyo Kijana Charles
Samuel (wa pili kushoto).
Afisa uhusiano
na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Charles
Samuel (wa pili kushoto), anayejishughulisha na ufundi wa umeme, kadi ya
pikipiki kama baadhi ya misaada aliyopatiwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel
‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Nakwa,
Babati mjini hapo jana. Wanaoshuhudia ni Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey
Sayore ( kulia), afisa mauzo kanda ya Babati Johnson Zephania (katikati) na
mama yake mzazi Charles Doris Kombe (kushoto)
Afisa uhusiano
na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Charles
Samuel (kushoto), anayejishughulisha na ufundi wa umeme, msaada wa vifaa mbali
mbali vya ufundi na pikipiki kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’,
katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Nakwa, Babati mjini hapo
jana. Wanaoshuhudia ni Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore (
kulia) na afisa mauzo kanda ya babati Johnson
Zephania (wa pili kushoto).
· Wajasiliamali kupatiwa vitendea kazi vya milioni 20 kila wiki na Airtel FURSA.
KMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA
imeendelea kutoa msaada kwa vijana mkaoni Manyara wenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 15 wakiwa na lengo la kutimiza dhamira yake ya
kuwawesha vijana nchini kuweza kujipatia kipato na ajira.
Akizungumza
Mkoani Manyara Meneja Mauzo wa Airtel Brighton Majwala amesema “Airtel
FURSA baada ya kuendesha semina ya Ujasiliamali mwezi uliopita
tulikutana na zaidi ya vijana 300 walijitokeza nakuzifahamu vyema FURSA
zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira. Leo hiii tumekuja kuwawezesha
hawa walioonyesha bidi zaidi”
Kwa
upande wake Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki ameeleza
kuwa “Airtel tuko tayari kutumia zaidi ya milioni 20 kila wiki
kuwawezesha vijana wanaojitokeza na kuonyesha wanania ya kujiendeleza
hapa nchini’.
Nae
kwa upande wake kijana Frank Rowland kutoka wilaya ya Hanang
aliyewezeshwa na Airtel Fursa alishukuru kwa kuwezeshwa na Airtel,
sitakaa bure, ntahakikisha ninauendeleza mradi huu unisaidie kimaisha na
kuwawezesha pia vijana wenzangu kupata ajira ntakazo wapa" alisema
Frank.
Kijana
mwingine aliyenufaika na Airtel Fursa ni fundi umeme, Charles Samuel,
mkazi wa mtaa wa Nakwa, Babati mjini, ambaye amepewa msaada wa pikipiki
na vitendea kazi vingine kwaajili ya kufanyia biashara ya kutembelea
wateja watakaohitaji huduma yake ya ufundi.
Charles
aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa usafiri na zana alizozipata
zitachochea mafanikio yake kimaisha na kuwataka vijana wenzake
kuchangamkia fursa zinazotolewa na Airtel ili waweze kuondokana na
umasikini
Mwenyekiti
wa Mamlaka ya Mji wa Katesh, wilaya ya Hanang, Michael Severine,
ameishukuru kampuni ya simu ya Aitel kwa kutimiza ndoto za vijana
kiuchumi kupitia mradi huo wa Airtel Fursa.
"Tulikuwa
tunaambiwa watu wanatoa hongo ili wapatiwe mitaji kwa njia ya
upendeleo, na Airtel lakini kwa kumwezesha kijana mjasiriamali wa
Hanang, tena kwenye kitongoji cha Katesh 'B", nimebaini kuwa ni uongo na
uzushi" aliongeza mwenyekiti huyo.
No comments:
Post a Comment