JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


DAWASCO KUZIMA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI.

Share This
TAARIFA KWA UMMA
KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI

SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO), LINAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU CHINI UTAZIMWA KWA SAA 36 KWA SIKU YA ALHAMIS TAREHE 18.02.2016. 

UZIMWA KWA MTAMBO HUO KUMETOKANA NA MATENGENEZO KATIKA BOMBA KUU LENYE UKUBWA WA INCHI 54 LINALOSAFIRI MAJI KUTOKA BAGAMOYO MPAKA KWENYE MATENKI YA MAJI YALIYOPO CHUO KIKUU ARDHI . 

MATENGENEZO HAYO YATAFANYIKA ENEO LA LUGALO JESHINI NA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI YA TAREHE 18/02/2016

KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YATAKOSA MAJI:

MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO. 

WASILIANA NASI KUPITIA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022-2194800 AU 0800110064

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU


“DAWASCO TUTAKUFIKIA”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad