JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


93.7 EFM RADIO KUTANGAZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA LIVE.

Share This
Katika kuendelea kuwapa burudani ya michezo wasikilizaji wake, Efm Radio kituo pekee kinachochambua michezo kiundani zaidi kitarusha moja kwa moja mchezo waligi kuu ya soka Tanzania bara ikiwani Dar es Salaam dabi ambapo bingwa mtetezi wa ligi hiyoYanga akiwa mwenyeji wa wekundu wamsimbazi Simba, katika mchezo utakaochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa10:00 jioni siku ya jumamosi ya tarehe 20/02/2016. 


Mchezo huo ni wa roundi ya pili ya ligi kuu ya soka ya Tanzania bara ambapo roundi ya kwanza Yanga ili ibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila mchezo uliochezwa katika uwanja huo wa taifa wakati samba akiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Kwasasa Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwaimecheza michezo 19 nakujikusanyia pointi 45 wakati wapinzani waoYanga wakiwa nafasi ya pili kwa kucheza michezo 18 nakujikusanyia pointi 43.

Kurushwa live Kwa mchuano huu kumedhaminiwa Na Michuzi blog, 


Bado nafasi ipo, iwapo unataka kutangaza nasi wasiliana kwa namba 0712 430 220, idara ya masoko ya Efm. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad