JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ZINGATIENI VIAPO VYENU – ANGELA KAIRUKI.

Share This
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki (Mb) akisalimiana na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Salome S.Kaganda (kushoto)  akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alipotembelea ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki amewataka watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuzingatia viapo vyao na kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao. 

Mhe. Waziri Kairuki amesema hayo alipotembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kukukutana na menejimenti na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo jijini Dar es salaam leo. 

“Nimekuja hapa kujionea na kujifunza juu ya taasisi yenu, nataka mfanye kazi msikiuke taratibu na sheria kwakuwa tu mna nafasi ya kuwa katika ofisi hii, mna jukumu la kuhakikisha mnatekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, taratibu na viapo mlivyokula,”alisema mhe. Waziri 

Aidha ameitaka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhakikisha jukumu la utoaji wa elimu ya maadili kwa umma linatiliwa mkazo kwani kufanya hivyo kutahamasisha maadili nchini na hivyo kufanya viwango vya juu vya maadili vinazingatiwa na kuongeza kuwa hali hiyo itawezesha viongozi kutenda haki, kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za umma na kuwa na huruma kwa wananchi. 

Mhe Waziri pia ameongelea kutokuridhishwa na mienendo ya viongozi wa umma baada ya kuacha utumishi ambayo haiendani na viapo walivyoapa wakati wakiingia katika nafasi zao na ameitaka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuangalia namna ambavyo jambo hilo linavyoweza kudhibitiwa na hivyo kuimarisha uwajibikaji wa pamoja. 

Mhe. Kairuki alikuwa katika ziara zake za kutembelea taasisi zilizoko chini ya ofisi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad