JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MHANDISI RONALD LWAKATARE ATEULIWA KUWA KAIMU MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA DAR ES SALAAM (DART).

Share This
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - TAMISEMI
TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali namba 120 la 2007, amemteua Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.

Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad