JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TIMU YA KILUVYA UNITED YAITUNGUA AFRICAN LYON KWA MABAO 2-1 LIGI DARAJA LA KWANZA

Share This
NA VICTOR MASANGU.
KIVUMBI cha ligi daraja la kwanza (FDL) kwa msimu wa mwaka 2015-2016 kinazidi kushika kasi ambapo timu ya Kiluvya United (Wabishi wa Pwani) jana iliweza kuifunga timu ya African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopingwa katika uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa Kundi 'A' ulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kila timu kucheza kufa na kupona kwa lengo la kuweza kuibuka na ushindi na kujinyakulia pointi tatau muhimu ili iweze kujiwekea mazingira mazuri ya katika msimamo wa ligi hiyo ya daraja la kwanza ambayo imeonekana kuwa upinzani wa hali ya juu kwa timu zote hususan katika kundi 'A'.

Kipindi cha kwanza katika dakika za mwanzoni wachezaji wa pande zote mbili walionekana kuanza mchezo huo kwa kasi kwa kuanza kushambuliana kwa zamu ambapo timu ya Kiluvya united iliweza kuandika bao la kwanza kunako katika dakika ya 23 lililowekwa kimiani na mshambuliaji Kassim Kilungo.

Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Africa Lyon na kuonekana wamebaki wameduwaha huku mashabiki wa kiluvya united waliokwenda uwanjani hapo wakiendelea kushangilia kwa staili ya aina yake ambayo iliweza kuwafurahisha wadau na wapenzi wa soka waliofika kushuudia mpambano huo.

Dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza timu ya African Lyon nayo iliweza kufanya shambulizi la kushitukiza ambalo liliweza kuzaa matunda kwa kuandika bao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji Kasakala Ndela baada ya safu ya ulinzi ya Kiluvya united kujichanganya katika eneo la hatari.

Kikosi cha wachezaji wa kiluvya kiliweza kujipanga upya na kuyarekebisha madhambi yaliyotendeka na kuanza kuliskama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la pili katika dakika ya 44 lililofungwa na mchezaji Ayoub Lipat baada ya kuunganisha mpira safi kwa njia ya kichwa.

Hadi kipinga cha kipindi cha kwanza kinapulizwa timu ya Kiluvya United ilikwenda mapumziko ikiwa iko mbele ya mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao timu ya African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, ambapo kipindi milango ya timu zote mbili ilikuwa migumu na kufanya hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Kiluvya kutoka kifua mbele kwa ushidi huo.


Kwa matokeo hayo Kiuvya United Wabishi wa Pwani kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 16 huku nafasi ya kwanza ikikamatwa na timu ya Ashanti United ya Jijini Dar es Salaam yenyewe ikiwa na pointi 18.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad