Uhaba wa usafiri wahatarisha usalama wa Abiria, kama walivyonaswa na kamera ya mtaa kwa mtaa leo jijini Dar es Salaam. 
Mwendesha Baiskeli ya Magurudumu Matatu Maarufu kama Guta Akiwa amepakiza Wachuuzi wa Matunda katika Barabara ya Uhuru Kariakoo jijini Dar es salaam.
Mwendesha Baiskeli ya Magurudumu Matatu Maarufu kama Guta akiwa amempakiza Mchuuzi wa Matunda aina ya Nanasi akiwa amening'inia nyuma ya Guta hilo ambapo ni Hatari kwa Maisha yake, leo kama alivyonaswa jijini Dar es Salaam.
Mwendesha Baiskeli ya matairi matatu maarufu kama Guta akiwa amempakia mchuuzi ambapo ni sehemu yake ya kujitafutia kipato chake cha kila siku leo jijini Dar es Salaam.
Kila mtu anaukaaji wake katika Baiskeli ya Magurudumu Matatu Maarufu kama Guta.
Mjasilia mali akiwakatika harakati za kujipatia kipato chake cha kila siku kama alivyo naswa na Kamera ya Mtaa kwa Mtaa leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ambayo sio rasmi kuvukia watembea kwa miguu ambayo inaonekana nihatari kwa usalama wao, Kamera ya Mtaa kwa Mtaa ya nasa leo jijini Dar es Salaam.
Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yamnasa mwendesha Pikipiki maarufu kama Boda boda akivunja sheria za Barabarani kwa kupita upande ambao si rasmi, na kutokujali kuvaa kofia ngumu maarufu kama Helment ambapo ni hatari kwa usalama wake leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii).



No comments:
Post a Comment