JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

Share This
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
   “PRESS RELEASE” TAREHE 12.11.2015.

MWANAMKE MMOJA MKAZI WA HORONGO MBEYA VIJIJINI AMEKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.

MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA HORONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUCY YESAYA [22] ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA USONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO KIJIJI CHA IZUMBWE SOKONI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.  

CHANZO CHA KIFO CHAKE NI BAADA YA KUPIGWA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA USONI. KIINI CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MPANDA BAISKELI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 28 ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.838 AAC AINA YA TOYOTA HIACE ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE DEO MBILINYI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 16:40 JIONI HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO HILO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PROMIS DANK MKAZI WA BWAWANI WILAYA YA CHUNYA ALIFARIKI DUNIA NJIANI AKIWA ANAPELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA RAILWAY, MTAA NA KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, MTOTO HUYO BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA HICHO AMBACHO KILIKUWA WAZI, ALIOKOLEWA AKIWA HAI LAKINI ALIFARIKI DUNIA AKIWA NJIANI KUELEKEA HOSPITALI TEULE YA MWAMBANI KWA MATIBABU.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI HASA KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

 AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYOWAZI, KUFUKIA MASHIMO YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA MSIMU HUU WA MVUA ZA VULI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad