JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NSSF WATOA SEMINA KWA WENYEVITI WA VYAMA VYA MSINGI (AMCOS) VYA WILAYA YA KILWA-LINDI

Share This
Wakulima wa Korosho wa Kilwa Masoko wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa Semina.
Afisa Ushirika wa Vyama vya Wakulima (AMCOS) Bwana Vincent Mhengilolo akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Ushirika wakati wa Semina iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF).
Mkulima wa Korosho wa Kilwa Masoko akiuliza swali ili kupata ufafanuzi kuhusu Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima Mjini Kilwa Masoko.

 SHIRIKA la Taifa la Hifadhi yaJamii(NSSF) limetoa Elimu kwa Wenyeviti na Makatibu wa Wakulima wa Korosho na Ufuta wa Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi kuhusu mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima, Mpango huo unamwezesha mkulima kupata mikopo mbalimbali ikiwemo mkopo wa vifaa vya kilimo pamoja na pembejeo za kilimo.

Aidha mpango huo unamwezesha mkulima na familia yake kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF yakiwemo mafao ya matibabu ambapo mkulima atapata matibabu bure yeye na familia yake. 


Wanyeviti na Makatibu hao waliweza kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina kuhusu Mpango huu kwa Wakulima na jinsi ya kuwasaidia Wakulima kuondodokana na gharama za matibabu kupitia mafao ya matibabu yatolewayona na NSSF.
 Afisa Mafao wa Shirika la Taifa la Hfadhi ya Jamii NSSF Bi Lydia Ignas akitoa ufafanuzi kuhuhu mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi Bi Nour Azin akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wakulima  kuhusu mpango  wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima katika semina iliyofanyika Kilwa Masoko Mkoani Lindi.
 Ofisa Mafao wa NSSF, Kabonwa Kandoro akiwaandikisha uanachama Wenyeviti na Makatibu wa vyama vya wakulima AMCOS baada ya semina iliyofanyika Kilwa Masoko mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad