JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WASICHANA WAPEWA KIPAUMBELE NA TAASISI YA DON BOSCO NET-TANZANIA KWA KAMPENI "BINTI THAMANI"

Share This
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania Fr. Celestine Kharkongor akizungumza na mwandishi wetu katika kituo cha Don Bosco Oystabay jijini Dar es Salaam kuhusiana na wasichana kutokubweteka na kukaa nyumbani kulea familia bila kuwa na mafanikio au ujuzi wao wenyewe kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.
Afisa Mipango wa Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania, Rosemary Njoki akizungumza  leo katika kituo cha Oystabay jijini Dar es Salaam.

TAASISI ya Don Bosco Net-Tanzania yahamasisha wasichana katika kujiendeleza kimapato na kimawazo kutokana na wasichana wengi kuona baada ya kumaliza elimu zao kama wamebaki na jukumu moja tuu la kulea familia taasisi hiyo imeaanda mafuzo kwaajili ya wasichana katika mikoa ya Dar es Salaam, Iringa na Dodoma.

Taasisi hiyo ambayo imesajiliwa na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi, VETA, inatoa vipaumbele kwa wasichana na imeandaa kampeni maalum kwaajili ya wasichana ijulikanayo kama BINTI THAMANI ambayo inataka kumkwamua msichana kiuchumi pamoja na kimawazo.

Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania, inatoa mafunzo mbalimbali wa wasichana ambayo ni Ufundi umeme, uchomeleaji vyuma, kuchora, ujenzi majengo, utengenezaji wa magari yaliyoharibika pamoja na ufundi wa umeme.

Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania, Celestine Kharkongor wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo katika kituo cha taasisi hiyo ya Oystabay jijini Dar es Salaam.

Pia amesema kuwa taasisi hiyo inatoa mafunzo ya ushonaji, mafunzo ya Saluni pamoja na upishi kwa wanafunzi waliomaliza Dalasa la Saba ndipo mwanafunzi huyo anaweza kujiunga na kozi nyingine ambazo hutolewa na VETA.

Nae Afisa Mipango wa Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania, Rosemary Njoki amewasihi wa wasichana na jamii kwa ujumla kuwa wapanue mawazo yao hasa katika jamii hii ya sasa ambapo msichana baada ya kumaliza masomo yake na kulea familia,  achukue ujuzi ambao atakua nao yeye mwenyewe ili aweze kujitegemea na kutokutegemea vitu vya kuletwa tuu.

Njoki amesema kuwa wasichana ambao wanaona kuwa elimu zao zimeishia hapo suluhisho ni kujiunga na Taasisi Tasisi ya Don Bosco Net-Tanzania iliyopo karibu nae ambapo hutoa elimu mbalimbali pamoja na ujasilia mali ili msichana aweze kujikwamua mwenyewe na si kutegemea mtu mwingine, aidha alisema kuwa taasisi hiyo imeshaanda kutoa fomu za kujiunga na mafunzo hayo ambapo mafunzo yataanza Januari 24, 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad