JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMPUNI YA SKYLINK WATANGAZA YASHINDI WANNE WA SHINDANO LA KUNUNUA TIKETI

Share This
 Bw. Moustafa H. Khataw kutoka kampuni ya Skylink akiwakaribisha waandishi wa habari pamoja na wageni waliofika katika droo ya kuwapata washindi wanne leo kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Bw.Husain AlSafi kutoka Emirates ambao walikuwa ni wadhamini wa shindano akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo katika ofisi za Skylink.
Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Bw. Abdallah Hemed akizichanganya vipeperushi ili kuwapata washindi wa droo hiyo.
Mwandishi wa habari kutoka TBC akiwa ameshika moja ya kipeperushi cha mteja wa Skylink aliyeibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia gari mpya aina Hyundai ix35   katika droo iliyochezeshwa  kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Skylink Solomon Mwale akiwatangaza washindi waliopatikana kwenye droo iliyofanywa na kampuni ya Skylink leo.
Mfanyakazi wa kampuni ya Skylink wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hyundai ambao walikuwa ni wadhamini mkuu kwenye shindano hilo
Waandishi wa habari wakiwa kazini

HASSAN Taliki mkazi wa  Jijini Dar es Salaam leo ameibuka mshindi na kushinda gari mpya aina Hyundai ix35   katika droo iliyochezeshwa  kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.

Mshindi huyo amepatikana kutokana na kukata tiketi ya ndege katika Kampuni hiyo hivyo ili aweze kupata zawadi hiyo ametakiwa kwenda na kipeperushi Skylink cha tiketi aliyokana na kitambulisho chake kwa maelekezo zaidi.

Washindi wengine walioshinda kwenye droo hiyo ni  Mohamed Swala ambaye  ameshinda safari ya kwenda Mahinra  kwenda na kurudi huku Issa Nassoro ambaye amekuwa mshindi wa tatu  amepata tiketi ya kwenda na kurudi Dubai ambako atapelekwa na Kampuni hiyo .

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Ofisa wa Skylink Solomon Mwale  alisema kwamba wamepanga kufanya hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao ili umma uweze kuamini kwamba hawabahatishi na droo ikichezeshwa inakuwa  ni kweli.

Droo hii ni sehemu ya motisha inayotolewa na Kampuni yetu  kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.

Droo hiyo imedhaminiwa na Skylink, Hyundai, Emirates, Exim Bank na Club Mahindra.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad