WIKI ya nenda kwa usalama ni muhimu katika jitihada za kuboresha masuala ya usalama barabarani ikiwa ni jambo lililo na kipaumbele katika ajenda za kitaifa nchini Tanzania.
Wiki hii inatoa misingi ya kufanya kazi kuelekea katika kufikia maono na matarajio ya mazingira salama na kuboresha usalama barabarani.
Hivi karibuni mwenyekiti wa tume ya usalama barabarani bwana Elifadhili Mgonja wakati akiongea na waandishi wa habari katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama jijini Dar es salaam yaliyo fanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mwaka 2015/16 alisema kuwa ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo kikuu cha kupoteza maisha na mali nchini Tanzania. Ajali hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha vifo na ulemavu ambao unasababisha kudumaa kwa maendeleo ya watu kiuchumi na kuathili uchumi wa taifa kwa ujumla.
Upigaji vita ajali za barabarani nchini limekuwa ni suala linalopewa kipaumbele kwani ajali mbaya zimekuwa zikiendelea kutokea. Pamoja na sababu nyingine, miundombinu mibovu, uchovu kwa madereva, uchakavu wa magari kama kukosa breki kutokana na kutokuwa na matengenezo imekuwa ni chanzo kikuu cha ajali mbaya nchini Tanzania.
Kwa nyakati tofauti, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni katika ofisi za kampuni ya Diamond Motors Ltd (Hansa) iliyopo katika barabara ya Nyerere, meneja mkuu (masoko) wa kampuni hiyo Ndugu Laurian Martin aliwaasa watanzania kuweka kipaumbele katika “usalama kwanza”.
Aliongeza kwa kusema kuwa utumiaji wa magari yaliyoboreshwa katika teknolojia ambayo kwa sasa yanapatikana katika soko la Tanzania kama vile malori ya Fuso FZ an Fuso FJ yanatoa nafasi kubwa ya kupunguza ajali za barabarani.
Martin aliongeza kusema kuwa “Malori ya Fuso FZ yanauwezo mkubwa wa breki zenye ukubwa, upana na unene unaolingana katika magurudumu ya mbele na ya nyuma, pia ina kifaa cha kujazia upepo pamoja na matanki ya kuhifadhia yanayokuhakikishia usalama wa hali ya juu katika miundombinu ya Tanzania na masafa marefu.
Malori haya pia yana vifaa maalumu sehemu ya mbele kwaajili ya kuzuia gari isianguke na kubilingika kirahisi ikiwa ni pamoja na mfumo wa matairi mpana unaoongeza ustahimilivu. Hivi ni vipengere muhimu sana hasa katika barabara mbovu na uendeshaji wa hali iliyokithili.
Bwana Martin aliendelea kwa kusema kuwa uchovu kwa madereva pia unachangia katika ajali za barabarani hasa katika uendeshaji wa masafa marefu. Malori ya Fuso FZ kutoka Diamond Motors yana kibini iliyo ninginizwa vizuri katika mihimili yake ambayo inasaidia kupunguza mtikisiko hasa katika matuta ya barabarani, haipati joto wala makerele kutoka kwenye injini, pia ina kiti ambacho kina rekebishika pamoja na usukani unaoweza kurekebishika. Vipengele hivi vinampatia dereva unafuu wa kuendesha ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa kusababisha ajali.
Usalama barabarani ni muhimu sana kwa watanzania na hii inadhihirishwa kwa uwepo wa wiki hii ya nenda kwa usalama nchini Tanzania ikiwa ni nia thabiti ya kupunguza ajali za barabarani. Muunganika wa sababu mbali mbali za kiusalama ukizingatiwa inaweza kupunguza ajali za barabarani. Usimamizi wa usalama barabarani kutoka kwa washikadau wa sekta hii, mafunzo muafaka kwa madereva ikiwa ni pamoja na utumiaji wa magari yaliyoboreshwa kwa ubora kama vile Fuso FZ na Fuso FJ ambayo hayahitaji matengenezo ya mara kwa mara na yametengenezwa kwa teknolojia iliyoboreshwa katika kumpunguzia dereva uchovu na ubora wa kuhimili miundombinu ya Tanzania inaweza kuchangia katika uboreshaj wa usalama barabarani.
Kuhusu Diamond Motors Limited (Hansa Group)
Diamond Motors Limited imekuwa wasambazaji pekee wa malori ya Fuso nchini kwa zaidi ya miaka 30. DML imeweka rekodi katika secta ya magari, kwa kufanya kazi kwa ushirikaino na makampuni ya magari yenye ubora wa hali ya juu zaidi duniani. Ushirika wao imara na makampuni yanayoongoza duniani kama vile magari ya abiria ya Mitsubishi kutoka Japani, matairi ya Yokohama kutoka Japani, MTU na ZF kutoka Ujerumani yameleta umaarufu na kutoa uwanja mpana wa wateja kutoka sehemu mbali mbali za ukanda huu.
No comments:
Post a Comment