TANZANIA na miaka 10 ya ukuaji wa kasi na kuimarika kwa sekta ya Mawasiliano
Na Semu Mwakyanjala, TCRA
KUMEKUWEPO na ukuaji mkubwa na mpana wa sekta ya mawasiliano nchini Tanzania kwa upande wa miundombinu na huduma ambavo kwa pamoja vimeleta faida kwa Watanzania katika miaka ya hivi karibuni. Sekta hii inaongozwa na Sera ya Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) ya mwaka 2003.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kwa kifupi TCRA, ni chombo huru cha Serikali kinachohusika na kusimamia sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini Tanzania na ina majukumu ya kutoa leseni kwa makampuni ya mawasiliano, ikiwemo ya huduma za simu, utangazaji, intaneti na posta na usafirishaji wa vifurushi.
TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Na 12 ya 2003 ambayo iliziunganisha zilizokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania na Tume ya Mawasiliano Tanzania. Tangu ilipoanza kutekeleza majukumu yake 1 Novemba 2003, TCRA iomekuwa ikiwashirikisha wadau wake muhimu kupitia mashauriano kwenye masuala mbalimbali.
Ukuaji imara na wa kasi wasekta ya mawasiliano nchini ni sehemu ya matunda yanayoonekana na Serikali ya Awamu ya Nne ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Sera nzuri za serikali na kufunguliwa kwa soko huria zimewezesha kuongezeka kwa wawekezaji na hivyo kuwapa watumiaji fursa ya kuchagua huduma bora wanayohitaji kwa gharama wanazomudu.
Kuanzishwa kwa mfumo wa leseni za muingiliano yaani (Convergence Licencing Framework) ambao ulianzishwa mwaka 2005 kutokana na kuendelea kukua kwa kasi kwa teknolojia kulikopelekea mwingiliano wa Teknolojia (Technological Convergence) kumechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa sekta ya mawasiliano.
Mfumo huu una aina nne za leseni ambazo ni:
Leseni ya Mitandao (Network Facility):
Inajumuisha miundombinu ya setelaiti, mitandao inayotumia waya aina ya optic fibre, uwekaji wa nyaya na njia za mawasiliano, vifaa vya mawasiliano kutumia redio, milingoti ya mawasiliano ya simu za mkononi, minara na vifaa vya kurushia matangazo ya vyombo vya utangazaji;
Leseni ya Mtandao wa Simu (Network Services):
Hii ni leseni inayoruhusu kutoa huduma za simu yaani sauti, picha na takwimu (voice, data, etc);
Leseni ya Huduma (Application Services):
Hii ni leseni inayoruhusu mmiliki kutoa huduma kama vile internet, kupiga simu kupitia internet, takwimu kwa ajili ya biashara, na huduma za kutuma taarifa fupi;
Leseni ya Huduma ya Maudhui ( Content Services)
Hii ni leseni inayoruhusu mmiliki kutoa huduma za utangazaji wa redio na televisheni na taarifa kupitia mitandao ( online publishing) na taarifa za habari.
Leseni chini ya mfumo wa CLF zinatolewa kwa ajili ya kutoa huduma katika ngazi nne- ngazio ya kimataifa, ya kitaifa, ya mkoa na wilaya.
Maendeleo tunayoshuhudia kwenye sekta ya mawasiliano nchini ni sehemu ya matokeo ya mpango mkakati wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa 2006/7 hadi 2010/11 na 2011/12 hadi 2015/16 ambao ulibuniwa na kutekelezwa Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi na kuwezeshwa na kuchangiwa na juhudi za watumishi wa Mamlaka ambao wanafanya kazi kwa bidii na weledi.
TCRA inatekeleza mpango mkakati sambamba na dira,dhima au dhamira na lengo kuu la Mamlaka.
Dira ya TCRA ni “Kuwa Mdhibiti mwenye hadhi ya kimataifa, kwa kuweka na kusimamia usawa katika haki na majukumu ya watoa huduma za mawasiliano na kuendeleza huduma zinazojali mazingira, na uwezo wa kiuchumi wa watumiaji.”
Dhima au dhamira ya Mamlaka ni “Kuwa na mfumo mahsusi wa usimamizi, kuboresha utendaji wa watoa huduma, na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kutoa mchango wetu kwa uchumi jamii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Lengo kuu ni” Kuendeleza ustawi wa Watanzania kupitia mfumo wa usimamizi wenye ufanisi na ambao unawezesha kupatikana kwa huduma za mawasiliano kwa wote”.
Soko la TEHAMA limekuwa kwa idadi ya watumiaji wa huduma hizo, kwa aina mbalimbali za huduma hizo na kwa kuongezeka kwa eneo ambamo huduma mbalimbali zinapatikana; ingawaje idadi ya watumiaji wa simu za mezani imepungua. Kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 sasa ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka 2008. Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii.
Sekta ya mawasiliano ni mojawapo ya sekta zinazoajiri watu wengi zaidi. Matumizi a simu za mkononi yamebadilisha mfumo wa maisha ya wananchi hapa nchini. Simu za mkononi siio tu kifaa cha mawasiliano 9 kwa kuongea na kutuma ujumbe mfupi au meseji0 lakini pia ni chombo cha kuimarisha watumiaji kiuchumi. Simu za mkononi zina matumizi ya aina mbalimbali ya kijitali kama vile huduma za fedha ambazo zinawawezesha watu kutuma na kupokea pesa. Watumaji wa huduma za fedha kuopitia simu za mkononi hivi sasa wanaweza kununua umeme, kulipia maji na kulipia huduma nyingine bila ya kuzalimika kwenda nje ya nyumba zao.
Watumiaji wanaweza kutoa pesa kwenye mashine za benki (ATM) na watu wengine wamejikomboa kutokana na adha ya kukaa foleni ndefu na kupoteza muda ambao wangeutumia chini ya mfumo wa zamani wa kibenki.
Wtumiaji wa huduma za benki kupitia mtandao wanaweza kuona miamala yao ikiwa ni pamoja na mishahara yao, wanaweza kuhamisha pesa kutoka akaunti ya benki kwenda pesa mtandao.
TCRA imefanikisha hili kwa kutopa namba fupi maalum kwa ajili ya miamala hii. Namba hizo ni ,*150*00# (M-pesa ya Vodacom), *150*01# (tigopesa ya Tigo), *150*02# (ezy-pesa ya Zantel), *150*60# (Airtel money ya airtel) na za mabenki kama vile *150*03# (CRDB simbanking), *150*20# (Barclays), *150*55# (NBC), *150*66# (NMB) na nyingine nyingi.
Kipindi cha miaka 10 iliyopita kinaweza kuelezewa kuwa ni Muongo wa Mapinduzi katika sekta ya Mawasiliano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mamlaka ya Mawasiliano imekuwa ikitekeleza kwa ufanisi Usimamizi wa Masafa ya Mawasiliano. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekuwa ikutumia kwa ufanisi mitambo minne ya kisasa iliyonunuliwa mwaka 2006/2008 ili kujiimarsiha na kujiongezea uwezo wake wa kupanga na kuthibiti matumizi ya masafa nchini. Hivi sasa kila ofisi ya Kanda ya Mamlaka ina mtambo (mobile frequency monitoring station) unaotumika kusimamia masafa katika kanda inayohusika. Kuwepo kwa mitambo hiyo kumepunguza muda wa kuchunguza na kumpangia muombaji masafa na kutambua kwa urahisi watumiaji haramu wa masafa na kuelewa mahali walipo; na kuzuia muingiliano (harmful interference) baina ya watumiaji wa masafa hivyo kuongeza ubora wa mawasiliano nchini.
Aidha, Mitambo iliyoko Dar-Es-Salaam imeboreshwa kwa kuwekwa “software” mpya na hivyo kuipa mitambo hiyo uwezo mkubwa na na ubora zaidi wa kusimamia masafa.
Baadhi ya mitambo ya kusimamia masafa iliyonunuliwa na TCRA
Mafanikio mengine muhimu kwenye sekta ya mawasiliano nchini ambayo msimamizi wake ni TCRA ni ufungaji wa mtambo wa kufuatilia mawasiliano ya simu, yaani Telecommunications Traffic Monitoring System, kwa kifupi TTMS.
Mtambo huu, ambao ulizinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete February 2014 una faida kubwa tano; ambazo ni kuwa na uwezo wa kujua mapato yanayopatikana kwenye simu za kimataifa;kuongeza mapato kwa sekta ya mawasiliano kutokana na simu kutoka nje ya nchi ili kuweka uwiano ulio sawa kati ya makampuni ya Tanzania na yale ya nje ya nchi. Mtambo huu utawezesha kuwekwa kwa uwiano sawa katika kutoza gharama za simu zinazoingia kwenye nchi husika kutoka nje. Hivi sasa nchi za Afrika zina viwango vya chini vya gharama za kuingia simu kutoka nje.
Hii imefanya makampuni ya hapa nchini kupata viwango vidogo vya mapato ukilinganisha na makampuni katika nchi nyingine. Kutokana na hili makampuni ya nchini na serikali wamekuwa wakipata mapato kidogo tofauti na ambayo wangepata kama kungekuwa na usawa wa bei kati ya kampuni za Tanzania na za nchi za nje.
Tofauti ya gharama hizo inaingia mikononi mwa wajanja wanaopitisha simu kinyemela.
Kwa kurekebisha kasoro hii wadau wa sekta nzima ya mawasiliano, yaani makampuni ya simu na Serikali watafaidika na huu mgao mpya wa mapato. Makampuni ya simu yataona ongezeko la mapato kutoka kwenye simu za nje na serikali itanufaika na mapato ya moja kwa moja pamoja na kodi za “corporate tax” ambazo zitaongezeka kwa kuwa makampuni ya simu yamepata mapato zaidi. Mtambo utaiwezesha serikali kupata shilingi bilioni 20 kwa mwaka kutokana na simu za kimataifa.
Faida nyingine ya mtambo hu ni kuweza kuzuia matumizi ya simu bila leseni kwa ajili ya kuunganisha simu za kimataifa na hivyo kuikosesa Serikali na Makampuni ya simu mapato halali. Mtambo pia utaongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya mawasiliano.
Mtambo utaiwezesha Serikali kupitia TCRA kusimamia sekta ya Mawasiliano vizuri.
Uthibiti na ukomeshaji wa upigaji na upokeaji wa simu kutumia mitambo ya mafichoni utaongeza ubora wa mawasiliano ya simu hivyo kuwapa watumiaji huduma bora.
Mtambo pia unaiwezesha Serikali kuwabaini wale wote wanaotumia mitandao ya kimataifa bila leseni hivyo kuikosesha Serikali mapato yake.
Aidha mtambo utawezesha Serikali kujua muda unaotumika kupiga simu nje ya nchi ya muda wa kupokea simu kutoka nje ya nchi. Kabla ya kufungwa kwa mtambo huu, TCRA ilikuwa inategemea takwimu kutoka kwa makampuni ya simu za mkononi.
Hata hivyo mtambo huu hausikilizi mazungumzo ya mtu yeyote. Mtambo huu unafuatilia mawasiliano ya simu ili viwango kamili viweze kulipwa na kukusanywa na Serikali iweze kupata mapato ya kuweza kuwahudumia vyema Watanzania.
TCRA pia inasimamia masuala ya usalama wa mtandao wa mawasiliano kupitia intaneti. Mamlaka imeanzisha kituo cha usalama wa mtandao, yaani Computer Emergency Response Team (TZ-CERT). Kituo kinashirikiana na wataaalamu wa kitaifa na kimataifa kuhusiana na masuala ya usalama wa mtandao wa intaneti. Aidha, Mamlaka inafanya kazi kwa karibu na vyonmbo vya usalama wa wananchi, hususan polisi katika kufuatilia matukio ya uhalifu kupitia mitandao.
Kimataifa, Tanzania mwanachama wa Shirika la Mawasiliano Ulimwenguni, yaani Telecommunication Union (ITU), lenye makao yake makuu Geneva, Uswisi. Vilevile kituo kinashirikiana na chombo cha kupambana na matukio ya uhalifu wa mtandao - Multilateral Partnership Against Cyber Threats (IMPACT) cha Malaysia.
Huduma za intaneti zimeenea kwa kasi na kuwezesha watumiaji kuwa na ufanisi katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Kusimikwa kwa nyaya za mawasiliaano ya kasi ambazo zimewekwa chini ya bahari ya Hindi na kuwa na vituo Dar Es Salaam kumeiwezesha Tanzania kuunganishwa na nchi nane majirani. Nchi hizo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, DRC Congo, Msumbiji na Zambia.
Nyaya hizo zimewekwa na makampuini ya SEACOM, EASSy na TEAMS na zimewezesha kuwepo kwa mawasiliano ya kuaminika, ya kasi, yenye ufanisi na ya gharama nafuu.
Watumiaji wa intaneti Tanzania wameongezeka kutoka 1.6 million mwaka 2005 hadi milioni 12 ilipofika Disemba 2014.
Matumizi ya intaneti yanafanikisha shughuli nyingi.
Mkongo wa taifa wa mawasiliano ni kama uti wa mgongo ambao utaiwezesha Tanzania kuimarisha mawasiliano na sehemu nyingine duniani.
Mkongo huu utafanikisha utoaji wa huduma kama vuile afya mtandao, serikali mtandao, kilimo mtandao na biashara mtandao.
Optic Fibre facility
Sekta ya Utangazaji Tanzania nayo imekuwa kwa kasi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Idadi ya vituo vya televisheni imeongezeka hadi kufikia 27. Ikumbukwe kwamba wakati Tanzania Bara inapata uhuru 1961 hapakuwa na kituo cha televisheni. Vituo vya redio vimeongezeka kutokakimoja mwaka 1961 hadi 97.
Tanznaia imekuwa nchi ya kwanza eneo la mashariki, kati na kusini mwa Afrika kuhamia kwenye mfumo wa tekinolojia wa dijitali. Vilevile imekuwa ni mojawapo ya nchi chache za Afrika ambazo zimehamia mfumo wa utangazaji wa dijitali.
Kwa kuhamia dijitali, Tanzania imeweza kufikia malengo ya yaliyokubaliwa nanchi zote duniani kuhamia mfumo huo ifikapo 17 Juni 2015.
Utangazaji wa televisheni wa dijitali una faida zifuatazo:
Sababu za kwenda dijitali ni:
· Mitandao yote ya Mawasiliano, yaani Mitandao ya simu, na mitandao ya Takwimu(internet)inatumia teknolojia ya dijitali.Ni mtandao wa utangaziji tu ndio unatumia teknolojia ya analojia. Teknolojia ya analogue imepitwa na wakati.
· Kutokana na mwingialiano wa teknojia (convergence of technologies)ya simu na utangazaji, mtandao wa utangazaji inabidi ubadilike.
· Kufaidika na faida nyingi zinatokana na teknolojia hii ya digital.
· Kwenda sambamba na makubaliano yaliyofikiwa na wanachama wa ITU – Geneva, 15/06/2006 kuwa mwaka 2015 ndiyo mwisho wa matumizi ya mfumo wa analogue kwa televisheni.
Kituo cha Mbeya FM Radio, ni kimojawapo cha vituo vya redio 115 nchini
Huduma za posta na usafikishaji wa vifurushi pia zinasimamiwa na TCRA. Watoa huduma kwenye sekta hii wameopngezeka kutoka mtoa huduma mmoja wa posta mwaka 1961 hadi watoa huduma 50. Hawa wanatoa huduma kwenye vipengele vya soko la kimataifa, Afrika Mashariki, kati ya miji na miji, na ndani ya mji.
Mpango wa Anuani Mpya za Makazi na Postikodi
(Postcode) ni mpango ambao utabadilisha anuani za
Watanzania kutoka sanduku la barua na kwenda namba
ya nyumba na jina la mtaa anaoishi mwananchi. Pia
maeneo wanaoishi wananchi yatapewa namba
maalumu za utalaamu wa posta (postcodes) ambayo
yataonyeshwa katika ramani za makazi ili kurahisisha
kutambulika.
Mpango huo ulizinduliwa Arusha 18 Januari 2010 na aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia ambaye sasa
ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza l
Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein. Awamu ya pili ya mpango ilpitekelezwa Dodoma Desemba 2010.
Changamoto kubwa ya mradi huu ilikuwa ni ukoswefu wa mipango miji na kuwepo kwa maeneo ya makazi yasiyopimwa.
Aliyekuwa Makamu wa Rais, Dr Ali Mohamed Shein katika uzinduzi wa Mradi wa Anuani ya Makazi na Misimbo ya Posta ( Post-Code Project) jijini Arusha 18 Januari, 2010. Mradi huu ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa. Wapili kulia, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Tekinolojia (mstaafu) Mh. Prof. Peter Msolwa.
Desemba 2013 TCRA ilitekeleza kwa mafanikio mradi huu kwenye eneo kama vile Keko, sehemu ambayo haijapimwa.
Utoaji wa majina ya mitaa na barabara umefanyika kwenye sehemu mbalimbali wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni, mkoa wa Dar Es Salaam.
Uwekaji wa Majina ya Mitaa ni muhimu kwa ajili ya anuani za Makazi. Juu Waziri wa Mawasiliani Sayansi na Tekinolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akitmbelea uwekaji wa majina ya mitaa wilayani Temeke, Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Postamasta Mkuu, Deos Khamis Mndeme , Kulia ni kurugenzi wa Masuala ya Posta Bibi Rehema Makuburi na anayetoa maelezo (aliyenyoosha mkono) ni Meneja wa Mradi huo Bwana Haruni Lemanya.
Mafanikio mengine muhimu kwa TCRA ni chini ya uonmgozi wa Awamu ya Nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la ghorofa 14 la makao makuu ya Mamlaka, Mawasiliano Towers barabara ya Sam Nujoma mjini Dar Es Salaam, hivyo kuwapatia watumishi wa Mamlaka sehemu muafaka ya kufanyia kazi na pia kuweza kupangisha ofisi kwa taasisi nyingine za serikali.
TCRA imefanikiwa kufikia viwango vya utendaji vya kimataifa na ilipewa hati ya ISO 9001:2008 na taasisi ya ACM ya Uingereza tarehe 30 Juni 2014. Hati hii ni kithibitisho cha ubora wa utoaji huduma na ufanisi wa kuhudumia wateja.
Mafanikio ya TCRA: Mkrugenzi Mkuu (mstaafu) wa TCRA Prof John Nkoma akipokea cheti cha Ubora wa Kimatafia ISO 9001: 2008 Certificate kutoka kwa Mkaguzi wa Kimataifa kutoka ISO, Ndugu Andrew Rowe kwenye jingo la Mawasiliano Towers Jijini Dar Es Salaam.
Ufunguzi wa ofisi ya Zanzibar ya Mamlaka ya Mawasilianop eneo la Chukwani Zanzibar na ofisi nyingine tano za kanda vimeiwezesha TCRA kuwa karibu zaidi na wadau katika maeneo yote ya Tanzania.
Ofisi nyingine ya Kanda ya Kati ambayo iko Dodoma, barabara ya Natron, eneo la Kisasa kwenye barabara kuu ya Dodoma – Dar Es Salaam the Dar Es Salaam Ofisi ya Kanda ya Ziwa kwenye jengo la NSSF, Barabara ya Kenyatta Mwanza, Kanda ya mashariki ambayo iko Mawasiliano Towers; Nyanda za Juu kusini kwenye jengo la Century Plaza, Mbeya na Kanda ya Kaskazini kwenye jengo la Summit, barabara ya Sokoine, Arusha.
TUZO: Kutokana na sera na mipango ya kuiendeleza sekta ya mawasiliano, Tanzania imeweza kupata tuzo mbalimbali na kuchaguliwa kuingia katika vyombo vya kimataifa vinavyoshughulika na maendeleo.
1. Tanznaia ilichaguliwa kuingia kwentye Baraza la Utendaji la ITU ( ITYU Council kwenye mkutano wa kila baada ya miaka mine uliofanyika Busan Korea Novemba 2014. Hii ina maana kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zinasimamia masuala ya mawasiliano duniani.
2. Mwaka 2006 na 2009 TCRA ilitunukiwa tuzo ya Msimamizi Bora wa Mawasiliano Afrika.
3. Umoja wa wasimamizi wa mawasiliano Afrika Mashariki ( EACO ambacho ni kifupi cha East African Communication Organisation uliichagua Tanzania kuwa nchi inayosimamia vyema zaidi mawasiliano Afrika Mashariki (“Best Regulator Country in East Africa) kwenye mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika Nairobi, Kenya Juni 2013.
4. Tarehe 1 Novemba 2013 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilituzwa cheti na Umoja wa Posta Duniani (UPU – Universal Postal Union) kwa kuwa na mfumo wa postikodi.
Sekta ya mawasiliano ni sekta mtambuka na ni chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mawasiliano ni mhimili mkubwa wa maendeleo ya taifa na matumizi sahihi ya huduma na bidhaa za mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya nchi.
|
Home
Unlabelled
TCRA , MIAKA 10 YA UKUWAJI WA SEKTA YA MAWASILIANO, TANZANIA
TCRA , MIAKA 10 YA UKUWAJI WA SEKTA YA MAWASILIANO, TANZANIA
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment