Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM
kilchofanyika katika ukumbi wa White house, Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015
katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na
kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwa katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti,
11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
Steven Wasira na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam
Kimbisa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya
CCM leo mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu, Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel
Nchimbi, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya
CCM leo mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu, Dk. Maua
Daftari na Samia Suluhu Hassan, wakibadilishana mawazo ukumbini, kabla
ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu, Adam
Kimbisa akiwasalimia wajumbe wenzake ukumbini kabla ya kuanza kikao cha
Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Shamsi Vuai Nahodha,
Zakia Meghji na Dk. Salim Ahmed Salim.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
Zakiah Meghji na Dk. Asha-rRose Migiro wakibadilishana mawazo ukumbini
kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCm leo mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ameir Pandu Kificho akibadilishana
mawazo na mjumbe mwenzake, Khadija Adood, kabla ya kikao cha Kamati Kuu
ya CCM kuanza leo mjini Dodoma.
Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzake wa Kamati
Kuu, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza leo mjini
Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment