Shindano
la kuibua na Kusaka Vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie
Talents (TMT) ambalo limedumu kwa takribani Miezi Minne hatimaye
shindano hilo linakaribia kufika tamati mnamo tarehe 22 August 2015 huku
Mshindi Mmoja Akiondoka Na Kitita Cha Shilingi Milioni Hamsini Za
Kitanzania.
Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.
Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.
Shindano
la TMT lilianza mapema mwezi wa Nne kwa kutafuta vipaji katika Kanda ya
Ziwa ambapo usaili ulifanyika Mkoani Mwanza na kuhitimishwa Kanda ya
Pwani Mkoani Dar Es Salaam kwa kupatikana Jumla ya Washindi 20 kutoka
Kanda sita za Tanzania.
Washindi
wa kanda sita walipata fursa ya kuingia ndani ya mjengo wa TMT huku
wakipatiwa mafunzo ya sanaa kutoka kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es
Salaam huku mchujo ukiendelea na kupelekea kila wiki Washiriki wawili
kuaga shindano, takribani wiki tano jumla ya washiriki 10 waliweza kuaga
shindano hili ambalo limefikia hatua ya kuwapata washiriki 10
waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora huku wakingojea fainali
itakayotoa mshindi wa kitita cha shilingi milioni hamsini za kitanzania
Mpaka
sasa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora wanaendelea na
kujifua Kwaajili ya fainali ambayo imebaki wiki moja tu kwa fainali hiyo
kuliteka jiji la Dar huku hofu na presha zikiwapata Washiriki hao.
Fainali
ya TMT itafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 22 August 2015 katika
ukumbi wa makumbusho ya taifa karibu na Chuo cha IFM kwa viingilio vya
shilingi Elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa viti vya kawaida.TMT
2015 inapigwa tafu na Precious Air, Cam gas, ITV na Radio One, Global
Publishers, I-View Studio, Paisha na Hussein Pamba Kali
No comments:
Post a Comment