JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA KWIMBA MKOANI MWANZA LEO

Share This
Sehemu ya Umati wa wakazi wa wilaya ya Kwimba na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara,Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu,Ndugu Kinana alikemea tabia ya wapinzania kuwahadaa vijana nchini kuwa wakiingia madarakani wataweza kuwatekelezea kila kitu,aidha aliwataka vijana wa kitanzania kuacha kabisa kuhadaika na baadhi ya Wanasiasa ambao wamekuwa wakiwapotosha na kuamini kila kitu kitapatikana bila kufanya kazi na kujituma.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba, ambapo aliitaka jamii wakiwemo mabalozi wa mashina kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), ili kuepusha mauaji dhidi yao.
Wananchi wilaya ya Kwimba wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba,Mh., Shanif Mansoor akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo. 
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa  CHADEMA katika Kijiji cha Ilula kata ya Ilula wilayani Kwimba,ndugu AmaraMateremki  akizungumza baada ya kuamua kukihama chama hicho na kuijunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akionesha baadhi ya kadi za wafuasi wa chama cha CHADEMA kuhamia CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikabidhi msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu Mjini Ngudu. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor pichani shoto.
Mmoja wa viongozi kutoka kikundi cha akina mama kiitwacha UAMSHO akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana mara baada ya kukabidhiwa vyerehani vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor .
 Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiongea kwa balozi wa shina namba 12,Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kwimba Ndugu Petro Ngh'ingi wakati wa mapokezi kwenye kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa Pichani kati ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba Bi.Tabu Lugwesa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor wakati wa mapokezi kwenye kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza.
 Walinzi wa Jadi wa kisukuma maarufu kwa jina la Sungusungu wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi ya jadi ya walinzi wa Kisukuma maarufu kama Sungusungu.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa kata ya hungumalwa waliojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji cha Mwamaya, Kwimba mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor akihutubia wakazi wa kijiji cha Mwamaya wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamaya waliojitokeza kwa wingi kumpokea kwenye wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha umeme kama ishara ya kuwasha umeme  kwenye nyumba ya Ndugu Charles Lusana mkazi wa kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa,Kwimba mkoani Mwanza.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Ndugu Charles Lusanamkazi wa kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa mkoani Mwanza mara baada ya zoezi la kuwasha umeme kukamilika
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma za utamaduni Idibuili wakati alipotembelea kijiji cha Hungumalwa kuona na kushiriki ujenzi wa Zahanati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilula Hamala Materemki, kata ya ilula wilani Kwimba aliyejiuzulu na kuamua kujiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Diwani ya kata ya Hungumalwa Shija Marando wakati wa kuona na kushiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hungumalwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Hungumalwa wakati wa kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya kijiji.Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor na Diwani wa Kata ya Hungumalwa Shija Marando.
 Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor akishiriki ujenzi wa zahanati ya Hungumalwa wilayani Kwimba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad