Meridianbet Tanzania
wameendelea na utaratibu wao wa kuwa karibu na jamii, kwa kutoa sapoti kwa
vijana katika shughuli zao za kuutafuta mkate wa kila siku. Tumu ya
Meridianbet, wikiendi iliyopita iliwatembelea boda boda na kuwaunga mkono
katika shughuli zao za utafutaji kwa kuhakikisha wanakuwa salama. Ikiwa ni
muendelezo wa kugawa nyenzo za usalama wa boda boda, baada ha kutoa kofia ngumu
na reflectors awamu iliyopita, wakati huu wametoa reflector nyingi zaidi kwa
vituo vitano vya boda boda.
Vituo ambavyo vilitembelewa na Meridianbet ni
Makumbusho, ambapo zoezi hilo lilianza likiongozwa na Twaha Mohammed kutoka
ofisi ya masoko ya Meridianbet, aliyeambatana na timu ya watu watatu wengine
kutoka kampuni hiyo.
Mwananyamala A, Mwananyamala kwa Kopa, Magomeni, Fire na Muhimbili ni miungoni mwa vituo vilivyonufaika na zoezi hilo la kampuni ya Meridianbet.
Wakati wa shughuli hizi, Meridianbet walisisitiza ni muhimu boda boda kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa ajili ya usalama wao, na wale wanawategemea.
"Tunagawa hizi kwa sababu tunazingatia umuhimu wa usalama wenu, kama vijana na watu ambao mnategemewa na familia zenu na watu wanaowapenda. Tunashauri muendelee kuwa makini barabarani, na kuzingatia sheria za usalama barabarani ambazo zinawahakikishia usalama ninyi na watumiaji wengine wa bara bara." - Twaha Mohammed
"Hawa ni vijana, wanafanya kazi nzuri kujitafutia kipato. Kuwa salama ni jambo la msingi, reflectors zinawasaidia kuonekana zaidi hata wakati wa giza. Sisi kama Meridianbet tunawaunga mkono shughuli zao kwa kuwasaidia kuwa salama zaidi, wakati mwingine tuligawa kofia ngumu, wakati huu tunawapa reflectors. Zoezi hili haliishii hapa." Shadrack Maarufu kutoka kitengo cha masoko
Meridianbet.
Boda boda kwa upande wao wanasema wanaona ni jambo jema, na ni faraja kwao kuona wanakumbukwa na kampuni mbali mbali katika masuala ya usalama wao.
"Mimi nawashukuru sana
Meridianbet, maana wanazingatia kuwa sisi vijana tunahitaji kuwa salama. Tunafarijika sana, natoa shukrani kwa niaba ya wenzangu. Na mida ya kubeti imewadia nitaenda kuchakata majamvi yangu"
No comments:
Post a Comment