JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB) KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MKOANI DODOMA

Share This

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) wakila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa kuwa Mawaziri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifatilia hotuba za viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) pamoja na Mawaziri wawili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri wa Fedha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad