JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Wazazi watakiwa kusomesha watoto wa kike na kuacha kuwaoza

Share This

Na Woinde Shizza, Michuzi TV Arusha
WAZAZI hapa nchini wameshauriwa kuhakikisha wanasomesha watoto wao wa kike ili waweze kuwa na mafanikio katika maisha yao badala ya kuwakatisha masomo na kuwaozesha kwa ajili ya kujipatia mali na kipato.

Rai hiyo imetolewa jana na mkuu wa mkoa wa Tabora, mstaafu, Agrey Mwanri ,kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya shule ya Green Valley, ya jijini Arusha ,maadhimisho ambayo yameenda sambamba na mahafali ya 5 darasa la saba na yasita kwa
Alisema kuwa haiwezekani watoto wa kike wasipate elimu kwa sababu ya kuozeshwa ,bali ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kipaumbele cha elimu ni kwa watoto wa kike.

Mwanri alisema wazazi wote ambao wanaokatisha masomo ya watoto wao wa kike kutokusoma hao ni wakatili wa hali ya juu na ukatili huo hauvumiliki wala kukubalika lazima Wasukumwe ndani kutokana na uonevu huo wa kiwango cha juu .


Alisema kuwa hayuko tayari kuona watoto wa kike wakikatishwa elimu kwa kisingizio cha kuozeshwa ,hilo atapambana nalo katika siku zote za maisha yake.

Alibainisha kama unataka kusaidia watu masikini na wanyonge ni kuhakikisha unasomesha watoto wa kike ambao wana jukumu kubwa la ulezi wa familia .


Aidha alibainisha kuwa sifa kubwa moja wapo ya elimu ni kwamba mtu akisha pata elimu hakuna anaeweza kuichukua au kuinyang’anya hata ukifungwa gerezani au kufariki unakufa nayo .


Aliupongeza Uongozi wa shule hiyo kwa kuweza kutoa elimu ambayo imewezesha wanafunzi mbalimbali waliosoma shule hiyo wamekuwa na mafanikio makubwa wakiwemo watoto wa kike.


Awali mmiliki wa shule hiyo Yahya Njarita, alisema kuwa shule hiyo katika kutoa elimu imefanikiwa kutoa wanafunzi wengi mbalimbali wakiwemo mmmoja ambae ni Rubani wa shirika la ndege nchini ATC,na mwingine ni daktari bingwa ICU muhimbili Idara ya watoto na wengine ni wataalamu katika nyanja mbalimbali ikiwemo wahandisi.


Alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha shule hiyo inakuwa na mafanikio makubwa katika elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad