JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ASILIMIA 75 YA TAKA HUZALISHWA NCHINI - NIPE FAGIO

Share This


Mabalozi kutoka Shirika la Nipe Fagio, Marco Dotto (kushoto) na Ali Hamisi (Kulia) wakiandaa taarifa za ripoti ya ukaguzi wa taka na chapa yaani, Waste and Brand Audit (WABA) wakati wa Siku ya Usafi Duniani iliyofanyika mnamo tarehe 19 Septemba mwaka huu katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.  

Mabalozi kutoka Shirika la Nipe Fagio,  Ali Hamisi (kushoto) na Marco Dotto  (Kulia) wakiandaa taarifa za ripoti ya ukaguzi wa taka na chapa yaani, Waste and Brand Audit (WABA) wakati wa Siku ya Usafi Duniani iliyofanyika mnamo tarehe 19 Septemba mwaka huu katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.


Na mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

MNAMO Septemba 19, Tanzania iliungana na nchi 179 kote ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani. Siku ya Usafi Duniani ni sehemu ya Let’s Do It Tanzania, kampeni ya kitaifa inayoongozwa na Nipe Fagio, shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi na jamii, sekta binafsi na serikali kufikia maendeleo endelevu katika sekta ya usimamizi wa taka.

Akitoa ripoti ya Siku ya Usafi Duniani 2020 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio, Bi Anna Le Rocha, ameshukuru mashirika yote yaliyojitokeza, wanajamii, na washiriki wote walioshirikiana na Nipe Fagio kufanya Siku ya Usafi Duniani ya mwaka huu kufanikiwa.

"Tunapotoa ripoti ya Siku ya Usafi Duniani ya mwaka huu, kwanza tunapenda kuwashukuru mashirika yote yaliyojitokeza, wanajamii na watu binafsi ambao wamejiunga na sisi na kufanikisha tukio hili muhimu.'' amesema.

 Amebainisha kuwa zaidi ya mashirika 250 katika sekta hiyo, na watu 4,621 wameshiriki katika shughuli za usafi nchi nzima.

Bi Anna ameeleza kuwa mwaka huu shughuli za usafi zilipapangwa kufanyika katika maeneo 25 na Mikoa 13 ya nchi. Katika maeneo 19 kati ya 25 ya kusafishwa, Ukaguzi wa Taka na Ukaguzi wa Chapa (Waste Audit and Brand Audit) ulifanywa kwa kukusanya data juu ya mjumuisho wa taka na mchango wa chapa mbali mbali katika uchafuzi wa mazingira wa taka za plastiki.

"Ni jambo la kusikitisha kwamba baada ya kufanya Ukaguzi wa taka na Chapa, tuliona tena kuwa asilimia 75 ya taka zilizokusanywa zinazalishwa na kampuni na viwanda vya hapa nchini, haswa chupa za vinywaji vya plastiki, vifuniko vya chupa za plastiki, mifuko ya plastiki na hata pakti za plastiki.'' ameeleza Bi Anna.

Amebainisha kuwa hiyo ni fursa kwao  katika  kushughulikia suala hilo nchini pamoja  na kupata suluhisho bora kwa kufanya kazi pamoja na sekta binafsi, serikali na asasi za kiraia.

Amesema kuwa ili kuifanya siku ya Usafi Duniani ni lazima iwe ya kufurahisha zaidi, Nipe Fagio ilizindua kampeni inayoitwa 'Plastiki Yako Mazingira Yetu', kwa harakati ya kuwaleta watu na mashirika pamoja kusaidia jitihada za kuweka vizuizi kwa uzalishaji na matumizi ya plastiki mara moja nchini.

"Tunatambua na kuunga mkono juhudi kubwa ambayo serikali ya Tanzania imefanya kuendeleza na kutekeleza marufuku ya mifuko ya plastiki na tunajivunia kuishi katika nchi ambayo imechukua hatua dhahiri kushughulikia uchafuzi wa plastiki." Ameeleza

"Kwa hivyo, kuanzishwa kwa kampeni ya Plastiki Yako Mazingira Yetu, itasaidia katika kushinikiza plastiki ya matumizi moja ibadilishwe na mifumo endelevu ya utoaji wa bidhaa ili kuhakikisha kuwa watu, wanafaidika, na sayari ziko katika usawa," Bi Anna amesema.

Amesema hadi kufikia Oktoba 10, karibu mashirika 70 yalikuwa yamewasilisha nembo zao na zaidi ya watu 100 walikuwa wamesaini fomu ili kuunga mkono kampeni ya Plastiki Yako Mazingira Yetu.

“Ikiwa bado tunahitaji msaada zaidi, ninasisitiza kwa mashirika ambayo hayajawasilisha nembo zao kufanya hivyo kupitia http://bit.ly/nflogoplastikiyakomazingirayetu na / au saini fomu ya Google kupitia http://bit.ly/nfsignplastikiyakomazingirayetu, ”ameongeza.

Utafiti unaeleza  kuwa, 80% ya plastiki inayoingia baharini hutoka katika mito na njia za maji na imethibitishwa kuwa sampuli zote za chumvi zilizojaribiwa ulimwenguni zina microplastics, ikimaanisha kuwa wanadamu sasa wanatumia microplastics, dutu hatari, mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad