JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Kampeni YA TCRA ya Mnada kwa Mnada yatoa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Share This

 Afisa wa Idara ya Uhamiaji akitoa huduma kwa mwananchi wakati alipotembelea banda la Uhamiaji katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Wananchi wakipata huduma ya usajili wa katika banda la vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Afisa wa TCRA akimuhudumia mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika Mnada wa Tangamano jijini Tanga.
 Mwananchi akiweka alama za kidole kwa ajili ya usajili wa laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

WAKAZI wa jijini Tanga   na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA  Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa wa Tanga kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 
Amesema Mnada kwa Mnada utadumu kwa siku tatu katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo itatoa fursa kwa wananchi wengi kufika kupata huduma za Mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Salum kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Salum amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Salum amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Salum

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad