JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Ubalozi wa Uholanzi, NEEC wazindua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana

Share This

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi, Beng’i Issa wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul wapili kulia wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini na wengine ni wakurugenzi na maofisa kutoka taasisi hizo. (Picha na Mpiga picha Wetu, Dar es Salaam).
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi, Beng’i Issa wa pili kulia akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini, wa pili kushoto ni Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul,kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza hilo, Suleiman Malela na kushoto ni Ofisa wa Ubalozi huo, Bw. Ulrich Juhudi. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
BARAZA la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi nchini wamezindua program ya mafunzo ya ujasiriamali na malezi ya biashara kwa vijana waliohitimu elimu ya juu katika juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira na kuchochea uchumi wa viwanda.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi, Beng’I Issa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yanawalenga  vijana 50 wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini kuanzia sasa hadi miaka mitano iliyopita ambao wana nia ya kuanzisha, kupanua na kuboresha biashara zao.

“Ni mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanaotaka kujiunga wanahitajika kuandaa michanganuo ya mawazo ya biashara katika maeneo ya utalii, kilimo, nishati mbadala na mazingira,”,  fomu za kujiunga zinapatikana katika tovuti ya baraza ya www.uwezeshaji.go.tz au zinapatikana katika ofisi za baraza hilo aliongeza kusema, Bi. Issa.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya wiki moja ambapo vijana hao watapata fursa ya kujifunza mambo ya ujasiriamali na kuingia kwenye biashara pamoja na mambo mengine watapata nafasi ya kuandika michanganuo yao itakayo shindanishwa ambapo washindi watatu watapatiwa zawadi.

“Vijana watakao chaguliwa katika program hiyo watapewa mafunzo ya siku nne juu ya mipango ya biashara kabla ya kuendelea na mchujo wa kutafuta washindi watatu ambao watapewa mbegu mtaji,” mshindi wa kwanza atapata milioni 10, wa pili milioni saba na mshindi wa tatu atapata milioni tano na washiriki wengine watanufaika na ushauri wa kitaalamu, alisema, Bi. Issa.

Bi Issa alifafanua kwamba mafunzo hayo yanalenga maeneo manne ambayo ni utalii, Kilimo, Nishati mbadala na mazingira ambayo ni maeneo yenye kuleta matokeo chanya kwa haraka katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kupambana na tatizo la ajira nchini.

Alisisitiza kwamba mafunzo hayo yanawalenga wahitimu hao wa fani mbalimbali ambao wakiingia kwenye biashara watafanya vizuri na kuanzisha makampuni yatakayopata maendeleo makubwa na kuweza kujiajiri na kuajiri wenzao.

Bi Issa alisema kwamba hii ni programu ya majaribio kwa kushirikiana na Serikali ya ya Uholanzi kupitia program hiyo na na baada ya mafanikio itapanuliwa zaidi. 

“Pamoja na program hii kuwa ya majaribio, sisi kama baraza tumekuwa tukiendesha mafunzo kama haya tangu 2013 kwa kushirikiana na taasisi zingine” kwa sasa ni mwendelezo wa program hiyo.

Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu kama moja ya njia madhubuti ya kuhamasisha ujasiriamali katika kupambana na tatizo la ajira hapa Tanzania.

“ Serikali ya Uholanzi inayo furaha kushirikiana na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kuhamasisha ujasiriamali kwa sababu kuna wigo mpana na fursa za biashara na kujiajiri,” alisema

Balozi huyo aliongeza kwamba kila mwaka kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanaingia kwenye soko la ajira lakini hawana ujuzi na uzoefu wa kutosha kuweza kumudu changamoto hizo za mahitaji ya soko hilo, kwahiyo mafunzo hayo ni muhimu kwao kuweza kuajiri kupitia ujasiriamali.

Alieleza kwamba hapa nchini kuna wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali ambayo yanahitaji vijana wenye ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira na biashara za uwekezaji.

Balozi Verheul alisema kwamba serikali ya Uholanzi inaona program hiyo inamaana kubwa na matarajio yake ni kwamba makampuni mengi kutoka Uholanzi wataweza kusaidia programu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad