728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 28, 2016

  JOHN LISSU KUZINDUA ALBAMU YA 'UKO HAPA' OKTOBA 3, 2016 JIJINI DAR.

  Mwibaji wa Nyimbo za Injili, John Lissu anatarajia kuzindua albamu yake ijulikanayo kwa jina la 'UKO HAPA' katika ukumbi wa CC Upanga jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mwimbaji Angel Bernard na Mercy Masika kutoka nchini Kenya. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

   Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwimbaji Lissu alisema kuwa maandalizi yameshakuwa tayari anawaomba Watanzania na wapenzi wa Muziki wa Injili kumuunga mkono ili kuhudhuria katika uzinduzi huo. Mwimbaji John Lissu aliongeza kuwa waimbaji wote wamefanya mazoezi ya kutosha hivyo mwenye shughuli ambaye ni (Yesu) anasubiri watu wakife siku hiyo ili aanze kazi yake. 

  Waimbaji watakao msindikiza John Lisu ni Pastor Safari Paul, Cosmas Chidumule, Glorious Celebration, Bomby Johnson, The Voice na Next Level. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huwa Media, Bw. Jacob alisema kuwa kila kitu kimesha kamilika kuanzia vyombo vya Muziki, muonekano wa Ukumbi na pia alitoa rai kwa watu wote kuwahi kwani saa nane kamili shughuli nzima itaanza. Ni Tarehe 3/2/2012 katika ukumbi wa CCC Upanga kwa kiingilio cha sh 5000/=.Muda ni Saa nane (8) Mchana.
  Mwimbaji Mercy Masika kutoka nchini Kenya akiongea machache.
  Mwimbaji Angel Bernard akiongea machache.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JOHN LISSU KUZINDUA ALBAMU YA 'UKO HAPA' OKTOBA 3, 2016 JIJINI DAR. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top