JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ETIHAD YAANZISHA HUDUMA YA MALEZI KWA WATOTO NDANI YA NDEGE.

Share This
 Kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za wateja wa Etihad, Turky Alhammadi, Makamu wa rais wa huduma za wateja Bw.Calum Laming na Makamu wa Rais wa Huduma na Mapokezi Sajida Ismail, wakikata keki katika sherehe za uzinduzi wa vifaa vya michezo ya watoto na malezi.
Watoto wakifurahia katika sherehe za uzinduzi wa vifaa vya watoto zilizofanyika Abu Dhabi.

WAKATI familia nyingi zikijiandaa kwa ajili ya kwenda mapumzikoni katika nchi mbalimbali, Shirika la Ndege la Etihad  limepiga hatua nyingine katika ubunifu  kwa kuajiri wasaidizi watakaosaidia kulea watoto ndani ya ndege na  kuweka vifaa maalumu vya michezo ya watoto wakati wote watakapokuwa safarini.

Mkusanyiko wa vifaa vya watoto ni huduma mpya katika shirika hilo, vifaa hivyo vitakavyojumuisha vitafunwa na michezo mbalimbali ya watoto vinalenga kuwaburudisha watoto watakapokuwa ndani ya ndege.

Vifaa hivyo, vimezinduliwa katika sherehe ya watoto ilioyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Sanaa na Uvumbuzi cha Shirika hilo mjini Abu Dhabi.

Katika ndege zinazoingia Abu Dhabi, kutakuwa na vifaa vya michezo kwa watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi miaka minane. Katika umri huo, vifaa hivyo vitajumuisha vijitabu vidogo, kalamu za rangi, karata na sura za bandia zenye rangi mbalimbali. Ndege zinakazotoka Abu Dhabi zitakuwa na sanduku maalumu la michezo hiyo litakaloongezwa vionjo zaidi.

Watoto wenye miaka 9-13 watakuwa na michezo ya rika lao kama vile; Chemsha bongo na uundaji wa maumbo mbalimbali, pia kutakuwa na makasha maalumu ya Abu Dhabi yenye kalamu rula, peni na vitabu vya nukuu.

Watoto wanaopenda michezo ya kompyuta na teknolojia pia watapata nafasi ya kufurahia filamu mbalimbali, vipindi vya runinga na programu za kisasa katika vifaa vya kidigitali na watakaosafiri umbali mrefu, watahudumiwa na wasaidizi waliopitia mafunzo maalumu. Wasaidizi hao walianza rasmi kuhudumu mwezi Septemba, 2013.

Makamu wa Rais wa  Huduma za Wageni katika Shirika la Etihad, Calum Laming alisema: “Tunaelewa ugumu uliopo wakati  wazazi wanaposafiri umbali mrefu na watoto, hii ndio sababu iliyotufanya kuandaa mazingira rafiki kwa watoto wanapokuwa safarini, pia ni sehemu ya juhudi zetu za kuboresha huduma za anga hasa kwa wanaosafiri kifamilia na watoto wadogo.”

 Vifaa vya watoto vimetengenezwa na kampuni inayotengeneza vifaa vya watoto ya Milk Jnr’s & KidWorks iliyopo Uingereza, ambayo ni mshirika wa kitengo cha Malezi ya Watoto- Etihad na Kitengo cha Maendeleo. Mradi huo pia unahusisha wahusika wa michezo ya watoto kama Simba kundai, Nyuki Zoe, Ngamia Jamool na Boo- Panda. Kampuni ya Milk Jnr’s & KidWorks imechapisha nembo za watoto zenye maumbo mbalimbali yanayowakilisha ardhi ya Abu Dhabi katika sare za wafanyakazi wa Etihad. 

Katika kuboresha huduma zake, Etihad itazindua huduma mpya ya chakula kwa watoto  Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa huduma za wateja Zoe Telfer alisema: “Lengo la mradi huu ni kupata suluhisho la changamoto ya kusafiri na watoto katika ndege zetu. Tunatoa huduma hii kwa safari ndefu na safari zenye umbali mfupi huku tukizingatia sifa za kipekee za Shirika letu.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad