728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 3, 2016

  BENKI YA NMB YAZINDUA MPANGO WA AGRIBIASHARA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA FEDHA KWENYE KILIMO.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker, Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Seif  Ahmed na Mkuu wa Kitengo cha biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Renatus Mushi  wakionesha bango la Kilimo Mpango Mzima linalojumiisha Pembejeo, Ukulima, Mazao,Uuzaji,Usindikaji na Usambazaji ulio bora, thabiti na wakisasa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na Benki ya NMB kuzindua biashara ya kilimo Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Renatus Mushi na kulia ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Seif  Ahmed.

  BENKI YA NMB imezindua mpango mkakati wenye thamani ya bilioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma zake za fedha kwa miaka mitano kwenye upande wa Kilimo.

  Mpango mkakati huu hususan unahusu kupanua huduma za fedha kwenye mazao zaidi ya kilimo – kutoka matano mpaka zaidi ya 12. Mpango huu utatoa fursa ya huduma za fedha sio tu kwa wakulima (kupitia mfumo wa vikundi na kwa mkulima mmoja mmoja), lakini vilevile utaongeza uzalishaji zaidi kupitia mnyororo mzima wa thamani katika kilimo – yaani tangu kwa mtoa pembejeo, mzalishaji (mkulima), mchakataji, msafirishaji, mfanya biashara (muuzaji wa jumla, wa rejareja, na wanje ya nchi).

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker, amesema kuwa benki yake inatambua umuhimu na nafasi ya sekta ya kilimo kwenye uchumi wa nchi hii, na ndiyo maana imechukuwa juhudi za makusudi kuboresha na kupanua huduma za fedha zinazolenga kuikuza sekta hii.

  Alisisitiza “Kwa kuzingatia umuhimu wa kuboresha sekta ya kilimo Tanzania, tunalenga kujenga mazingira na taratibu ambazo mkulima mdogo na washiriki wote kwenye mnyororo huu wa thamani wataweza kuboresha ufanisi: katika upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji kwa njia za kisasa (mbgu bora, mbolea, kutumia zana na nyezo mabalimbali za kilimo, n.k.), pamoja na ufanisi kwenye masoko. Yote haya yanawezekana kupitia kupatikanaji wa uhakika wa huduma za fedha kwemye kilimo.

  “NMB tunaona fursa kubwa sana kwenye sekta ya kilimo”, aliongeza. “Tunaamini kwa kuongeza ushiriki wetu kwenye sekta hii, kutakuwa na msukumo chanya kwenye maisha ya wakulima wetu na wote kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hii, na vilevile kutimiza malengo ya NMB”. Alisisitiza. Bi Bussemaker vilevile alisema kwamba NMB Tayari inawafikia wakulima wadogo wasiopungua 600,000 nchi nzima. Kwenye mpango mkatai huu mpya, benki hii sasa vilevile inawalenga wakulima wakubwa, wafanyabiashara wa pembejeo, wachakataji wa mazao ya kilimo, wafanyabiasha / wauzaji wa mazao na wahusika wengine wote kwenye mnyororo mzima wa thamani katika kilimo.
   Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Seif  Ahmed akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa biashara ya kilimo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker akionesha namna benki ya NMB ambavyo inajishughulisha na biashara ya mazao kwa wakulima wa mazao hapa nchini ambapo NMB  katika mpango huo mkakati wenye thamani ya mabilioni kwa ajili ya kuboresha huduma zake za fedha kwa miaka mitano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BENKI YA NMB YAZINDUA MPANGO WA AGRIBIASHARA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA FEDHA KWENYE KILIMO. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top