728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 14, 2016

  TRA YATOA MASHINE ZA EFD KWA WIZARA ZINAZOKUSANYA MADUHULI YA SERIKALI.

  MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) imegawa Mashine za Kieletroniki za EFDs tano kwa kila katibu Mkuu wa Wizara kwa ajili ya kukusanya maduhuli ya serikali kwa kutumia mashine hizo.

   Hatua hiyo imetokana na agizo la  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wizara zinazotoa huduma ziwe na mashine za EFD ili kuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa taifa.

   Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa ugawaji wa mashine hizo kwa taasisi za serikali zitasaidia kutunza  kumbukumbu katika kupanga maduhuli.

  “Mashine hizi ni lengo serikali katika kuhakikisha wananchi wanaopata huduma wanapata risiti kwa kutambua umuhimu wa kodi kwa huduma wanazopata”amesema Kidata.

  Aidha amesema mashine hizo ni mashine za kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa za kisasa katika kutunza kumbukumbu za huduma ambazo wanazitoa.

  Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah Mwandumbya amesema kuwa watawafundisha wakuu wa idara hizo jinsi ya kuzitumia.
  Imeandaliwa na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii.
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akimkabadhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya mashine tano kwaajili ya wizara yake ili kila wanapofanya malipo mbalimbali mapato ya TRA yakatwe.
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akionyesha Mashine za Kiletroniki za EFDs ya mfano kabla ya kugawa kwa mashine tano katika wizara zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, ambazo zitakuwa kwaajili ya kukusanya mapato katika wizara hizo.
   Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akitoa maelekezo ya Mashine za Kieletroniki mbele ya makatibu wa kuu wa wizara pamoja na wawakilishi wa wizara mablimbali jijini Dar es Salaam leo kabla ya Kuanza kugawa katika wizara zote za serikali.  Baadhi ya Makatibu wa kuu wa wizara wakikabidhiwa mashine za Kieletroniki za EFDs na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata jijini Dar es Salaam leo.


  Baadhi ya wawakilishi wa wizara mbalimbali za serikali wakiwa katika mkutano wa kukabidhiwa mashine za Kieletroniki za EFDs jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TRA YATOA MASHINE ZA EFD KWA WIZARA ZINAZOKUSANYA MADUHULI YA SERIKALI. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top