JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


IFIKAPO 2030 WAKAZI WA DAR KUWA MILIONI 10.

Share This
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKOA wa Dar es Salaam unatarajiwa kuwa watu milioni 10 ifikapo 2030 hivyo kunahitaji uboreshaji wa jiji katika  kuendana na idadi  watu  kuongezeka kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda(Pichani) amesema kuwa kutokana kuwepo kwa ongezeko la watu kila mwaka Serikali ilibuni mradi wa uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania.

Amesema ukuaji wa jiji la Dar es Salaam unakabiliwa na makazi yasiyopimwa kwa asilimia 70 hadi 80 hivyo kutokana na hali ya ukuaji wa kasi  wa jiji la Dar es Salaam na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoikabili dunia ni pamoja athari ya mafuriko yanatarajiwa kuongezeka katika jiji.

Makonda amesema katika kukabiliana na uongezeko mradi uendelezaji jiji la Dar es Salaam unatarajia kuanza mwaka wa fedha 2016 /2017  kwa kuanza kuboresha miundombinu na kujengea uwezo manispaa katika utoaji wa huduma katika kuweza kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kukabili majanga ya dharula yanayoweza kutokea katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa katika mradi huo utaangalia maeneo ya watu wenye kipato cha kidogo na maeneo yao yamejengwa kiholela, ujenzi wa miundombinu ya barabara inayoaunganisha Wilaya na Mkoa pamoja kuunganisha maeneo mbalimbali na ukanda wa mabasi haraka.

Amesema vigezo viliibua miradi kama ujenzi wa barabara zinazoingia katika barabara kuu za manispaa zote zenye urefu wa kilomita  65.6 katika kuweza kupunguza msongamano wa magari, ujenzi wa wa mitaro ya kutiririsha maji ya mvua zenye urefu wa kilomita 31.8 katika maeneo ya Mto Ng’ombe, Msimbazi, Gerezani Greek, Yombo pamoja na Kwashego ili kuweza kutatua changamoto za mafuriko.

Makonda amesema katika mradi watapandisha hadhi makazi yaliyopangwa kiholela katika kata 14 ambazo ni Tandale, Mburahati, Mwanyamala, Gongola Mboto, Kiwalani,Ukonga, Keko , Kilakala, Mbagala Kuu, Mbagala, Mtoni , Yombo Vituka ,Kijichi pamoja na Makangarawe  kwa kujenga barabaza za lami zenye urefu wa kilomita 145.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad