JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATOA TIKETI YA BURE KWA MTANZANIA

Share This
Mshindi wa tiketi ya bahati nasibu ya Shirika la ndege la Etihad, Elisante Ombeni (35) alipokuwa akijiandaa kusafiri kutoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar tayari kwa ajili ya safari yake mjini Abudhabi.

SHIRIKA la Ndege la Etihad ambalo ni shirika rasmi la ndege la nchi ya Falme za Kiarabu, lenye makao makuu Abudhabi, hivi karibuni lilipanua wigo wa huduma zake jijini  Dar es Salaam, ambapo katika kuadhimisha ujio wake hapa nchini, Shirika hilo liliamua kumzawadia mtanzania mmoja tiketi ya bure kwenda na kurudi Abu Dhabi. Elisante Ombeni (35), Mkazi wa Mbezi Beach aliibuka kidedea kama mmoja wa washindi wa bahati nasibu hiyo ambayo ilifanyika wakati wa hafla ya uzinduzi wa shirika hilo jijini Dar es salaam.

Ombeni alipata fursa ya kutembelea mji wa Abu Dhabi ambao pia ni mji mkuu wa nchi ya Falme za Kiarabu.

Akiwa mwenye furaha baada ya kukamilisha safari yake, Ombeni ambaye ni mwajiriwa wa Wizara ya Maliasili Idara ya wanyamapori, alilishukuru Shirika la ndege la Etihad kwa kufikisha huduma zao katika mji mkuu wa kibiashara, Dar es Salaam, nchini Tanzania.

“Nilipokelewa vizuri sana siku ya kuanza safari yangu, wahudumu wa ndege wa shirika hili wanakufanya uwe huru kuuliza chochote unachotaka”. Alisema katika mahojiano ya hivi karibuni jijini Dar es Salaam

Alisema ndege za Etihad ni kubwa na baada ya kufika Abu Dhabi alifikia kwenye ukumbi maalum wa shirika la ndege hiyo ambao mteja anapatiwa huduma zote muhimu kama vile chakula, sehemu ya kupumzikia, kuoga, huduma ambazo zote ni bure.

Akiwa mjini Abu Dhabi Bw. Ombeni alishuhudia fursa nyingi za biashara kama;-magari, nguo, utalii na biashara ya vyakula. “Watanzania hawana budi kutembelea mji huu kwani ni dhahiri kuna mengi sana ambayo mtu binafsi anaweza kujifunza na kuyafanya hasa fursa za kibiashara ni nyingi sana” aliongezea.

Kwa upande wake Mratibu wa Masoko wa shirika la ndege la Etihad nchini Tanzania Bi. Grace Kijo alifafanua juu ya dhamira ya shirika la ndege hiyo na jinsi lilivyojipanga katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.

“Shirika la ndege la Etihad linafanyakazi kuhakikisha linajenga mazingira tulivu na ya uhakika kwa wateja kwa kutoa huduma bora za kuaminika kimataifa katika sekta ya usafiri wa anga”.

Alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wateja wao kuhusiana na bei nzuri za viwango vya ushindani za shirika hilo sambamba na urahisi wa kukata tiketi kwa njia ya mtandao.

Shirika la ndege la Etihad lilianzisha rasmi huduma zake hapa nchini mosi Desemba 2015 ambapo ni juhudi za shirika hilo katika kupanua wigo wa huduma zake Afrika likiwa tayari limeshafungua matawi mjini Nairobi, Kenya na Entebbe Uganda.
Shirika hilo kwa sasa linatoa huduma za safari kila siku kati ya Dar es salaam na Abu Dhabi ambao ni mji mkuu kwa Umoja wa nchi za falme za kiarabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad