JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


DC.MAKONDA AWAPA WIKI MBILI WATENDAJI WA KINONDONI KUSHUGHULIKIA UCHAKAVU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Share This
Mashimo wa Barabara eneo la soko la Mapinduzi kama panavyoonekana katikaka picha, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam alipotembelea na kuagiza patengenezwe haraka iwezekanavyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiangalia ubovu wa barabara ya Mwanachamala 'A' hadi Makumbusho jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua barabara ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza baada ya kukagua barabara hizo amewapa watendaji wa manispaa ya Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya magari yanayotumia barabara hiyo.

Amesema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujenga chini ya kiwango.

Makonda amesema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanatumia barabara hiyo ikiwemo na gari za kubeba.


Aidha amesema kuwa watahakikisha barabara zinafanyiwa maboresho katika urahishaji wa usafiri katika Manispaa ya Kinondoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad