JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


AIRTEL FURSA YAWAFIKIA VIJANA KISIWA CHA IRAMBA, KAGERA.

Share This
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kushoto), akimkabidhi kijana Joram Deus (wa pili kulia), mmoja wa vijana wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki katika ziwa victoria, msaada wa   msaada wa vifaa mbali mbali vya  uvuvi na mashua yenye injini mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kisiwani kwao Iramba, Kagera mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni ndugu wa vijana hao na wanakijiji wa eneo hilo.
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kushoto), akimkabidhi kijana Joram Deus (kulia), mmoja wa vijana wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki katika ziwa victoria, msaada wa msaada wa vifaa mbali mbali vya  uvuvi na mashua yenye injini mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kisiwani kwao Iramba, Kagera mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni ndugu wa vijana hao na wanakijiji wa eneo hilo.
 Kijana Joram Deus anayejishughulisha na uvivu wa samaki, akiangalia vifaa mbali mbali walivyokabidhiwa na Airtel Tanzania, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika  kisiwani kwao Iramba, Kagera mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni ndugu wa vijana hao na wanakijiji wa eneo hilo.

Airtel FURSA yawafikia vijana kisiwa cha Iramba, Kagera
·        Yatoa msaada wa zaidi ya Shs milioni 22 kuwawezesha vijana hao.

Kagera, Jumapili  20 Machi  2016Wiki hii Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa umeweza kuwafikia vijana wa kisiwa cha Iramba Mlumo mkoa wa Kagera wanaojishughulisha na uvuvi kisiwani hapo kwa kumuwezesha vijana Joram Deus na wenzie wawili vifaa bora vya uvuvi vyenye dhamani ya shilingi milioni 22, hatua inayotajwa kufungua mustakabali mpya wa maendeleo katika kisiwa hicho.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya makabidhiano katika kisiwa cha Iramba, Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki alisema, kuwezeshwa kwa vijana hawa kupitia Airtel Fursa ni ukombozi wa kiuchumi kwa familia zao na wakazi wa Iramba.

Airtel Fursa inatekeleza  wajibu wake katika kurudisha sehemu ya faida  kwa jamii ili kukidhi matakwa ya kiuchumi ama kijamii katika eneo husika hasa kwa vijana, na kuunga mkono jitihada za serikali katika kubadilisha maisha ya wananchi.

Nae mwenyekiti kijiji cha Iramba Mlumo, Novatus Bernado alisema “sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta za kiuchumi nchini Tanzania, sekta hii ilitazamiwa kukua kwa asilimia 5.3 hadi kufikia mwaka 2015, huku ajira rasmi na zisizo rasmi zikitengenezwa hususani kwa wakazi wanaozunguka maeneo ya vyanzo vya maji kama vile Ziwa, mto ama bahari.

“Wakazi wa Muleba uvuvi ndio shughuli zetu kuu kiuchumi, changamoto ya zana bora kwa shughuli hiyo ndiyo iliyomfanya kijana wetu Joram kuitikia wito wa kushiriki katika mpango wa Airtel Fursa ili apate kuwezeshwa kuendesha uvuvi wenye tija na kufungua milango zaidi ya kiuchumi na biashara kisiwani hapa.Tunawashukuru sana Airtel kwa kuweza kutuwezesha kwani imegusa uchumi wa kaya husika na pengine ikawa chachu ya ukuaji wa sekta ya uvuvi katika mwalo huu”

Akipokea  vifaa hivyo  Joram  ameishukuru Airtel Fursa kwa kuweza kubadilisha mtazamo wa biashara yao ya uvuvi, na kuwakumbusha vijana wengine kwamba vijana watoe fikira kwamba wengi wanaamini maisha mazuri na fursa za kiuchumi zinapatikana mjini tu ila wajue pale watakapo nyoosha mkono ndipo watakaposhikwa mkono na kuonyeshwa njia.

“Airtel fursa imefungua milango kwa sisi vijana na kutuwezesha kuyafikia malengo yetu yenye kukidhi mahitaji yetu na jamii inayotuzunguka.

Mpango huu ni wa kitaifa vijana wanapewa wito wa kuendelea kushiriki katika kuainisha fursa zao kupitia Airtel Fursa ili kuwezesha na kuyafikia malengo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad