JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAFANYAKAZI WA TANGA CEMENT WAFANYA USAFI SOKO KUU LA MJINI TANGA LA NGAMIANI

Share This
 Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga, Diana Malambugi (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifanya usafi katika Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani mjini humo leo, kuadhimisha Siku ya Uhuru iliyodhimishwa kwa watanzania wote kujishughulisha na shuhuli za usafi wa mazingira. 
  Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga, Diana Malambugi (kushoto) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Mwenyekiti wa Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani, Abubakar Shauri, baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya shughuli za usafi sokoni hapo leo, kuadhimisha Siku ya Uhuru ambayo watanzania nchini kote walijishughulisha na kazi za usafi wa mazingira.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga, wakifanya usafi katika Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani mjini humo jana kuadhimisha Siku ya Uhuru ambayo watanzania nchini kote walijishughulisha na kazi za usafi wa mazingira.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tanga Cement waliokwenda kufanya usafi katika Soko Kuu la Mji wa Tanga la Ngamiani, wakilisukuma trekta la kubeba takataka ili dereva wa gari hilo aweze kuliwasha na kuendelea na majukumu yake. 

 Baadhi ya wafanyakazi wa Tanga Cement wakifanya usafi katika soko la Ngamiani mjini Tanga leo. 
 Baadhi ya wafanyakazi hao wakiendelea na shughuli ya usafi katika soko la Ngamiani mjini Tanga leo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga wakipiga picha na baadhi ya watendaji wa Soko Kuu la Ngamiani mjini Tanga wakati wafanyakazi hao walipokwenda kufanya shughuli za usafi kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli kwa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru yatumike kwa shughuli za usafi wa mazingira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad