JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TUME YAWAASA WANANCHI KUTOSIMAMA KATIKA VITUO VYA KUPIGIA KURA

Share This
Na Anitha Jonas- Maelezo
7/10/2015
Dar es salaam
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini amewaasa wananchi kutosimama katika vituo vya kupiga kura mara baada ya kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kwani mawakala wa vyama vya siasa wa kuwepo katika vituo vya kupigia kura ili kulinda maslahi ya chama pamoja na wagombea wao.

Wito huo umetolewa na  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akifungua mkutano wa tume  na waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi nchini.

Jaji Lubuva amesema kuwa wajibu wa mawakala ni kuangalia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume zinazingatiwa katika mchakato mzima wa kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo na pia kulinda maslahi ya chama au wagombea wao.
“Changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ni pamoja na kuwapo na makundi ya vijana wanaohisiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kuwatisha wapiga kura hasa wakinamama ili wasiende kupiga kura”

“Ni rai yangu kwenu kuhakikisha hilo halijitokezi katika uchaguzi huu kwani kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania hivyo tusiruhusu vikundi vya watu kuwa  karibu na eneo la upigaji kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwani hii itapelekea uvunjifu wa amani” ameongeza Jaji Lubuva.

Mbali na hayo Jaji Lubuva amesema lengo la kushirikisha Jeshi la polisi kwenye uchaguzi mkuu ni kutambua na kuhakikisha kuwepo kwa hali ya usalama na amani wakati wa uchaguzi kwani uchaguzi huru na wa haki ni lazima uendeshwe katika hali ya utulivu na amani.

Kwa uapande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu amesema kuwa jukumu la jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, kuimarisha ulinzi katika vipindi vyote na haswa kipindi hiki cha uchaguzi, kulinda vifaa vya uchaguzi na kusimamia usalama katika vituo vya kupigia kura.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad