Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Kata ya
Kibada, Jimbo la Kigamboni, Amini Sambo akijinadi kwenye eneo la kata hiyo, Dar
es Salaam jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM,
Phares Magesa, (kulia) akimnadi Mgombea udiwani wa chama hicho kata ya Kibada,
Jimbo la Kigamboni, Amini Sambo eneo la Kibada, Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi Wetu
KAULI mbalimbali za hamasa kuelekea uchaguzi mkuu
zimeendelea kutawala majukwaani, huku jana Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM
wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema akiwavunja watu mbavu kwa vicheko na shangwe
baada ya kuifananisha ccm na mama mjamzito mwenye sifa na uzoefu wa kuingia na
kutoka salama siku zote kwenye chumba cha kujifungua yaani ‘leba’ huku upinzani
ukiambulia.. ‘poole’
Akiwanadi kwa mbwembwe Mgombea urais kwa tiketi ya ccm, John
Magufuli, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugulile na mgombea udiwani
wa kata hiyo Amini Mzuri Sambo, eneo la Kibada Dar es Salaam jana, Sikunjema
amesema historia ya CCM kuingia leba ya uchaguzi na kutoka salama inajidhihirisha
wazi
Alisema kwa mara ya kwanza Tanu ilifanikiwa kutoka leba
salama kwa kujifungua mtoto mzuri aliyeitwa Julius Kambarage Nyerere, baada ya
hapo ikaingia leba tena na kujifungua jembe la nguvu Ally Hassan Mwinyi,
ikaingia tena na kutoka salama na kipenzi chake Benjamin Mkapa, na kisha
tukatoka tena salama kwa kumpata mtoto rangi ya chungwa Jakaya Kikwete
Huku akishangiliwa na mamia ya wananchi wa Kibada Sikunjema
aliongeza kuwa katika kipindi chote hicho wapinzani kila wakitoka leba wamekuwa
wakiambulia…poooole, “ hawana uzoefu hata kidogo na leba cha uchaguzi”
Aliongeza, “mtaniwia radhi akinamama kwa mfano huu..ila
nataka nisisitize kuwa sote tunajua leba sio mahali pazuri, ukiingia kuna vitu
vinne vinaweza kutokea..ama ukatoka salama, au ukapoteza mtoto au ukampoteza
mama au ukapoteza vyote,..lakini ccm inajivunia kuwa na rekodi ya kutoka salama
katika leba za chaguzi kwa vipindi vyote.”
Aidha, mwanasiasa huyo machachari aliyeongozana na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya chama hicho, Phares Magesa, kwa mwaliko wa mgombea udiwani
wa kata hiyo Sambo, alihitimisha kwa kuomba kura za kutosha kwa wateule wa ccm
kwa ngazi zote
No comments:
Post a Comment