JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BAA YA BARACUDA, TABATA NA CHECK POINT YA CHANIKA WASHINDI WA WIKI WA FANYAKWELI

Share This
  Mkazi wa Baracuda, Tabata Gaston Arbogasti akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (kulia) kabla ya kukabidhiwa zawadi yake ya fulana na bia za bure katika hafla ya kuipongeza baa ya Baracuda iliyopo Tabata jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hii inaendelea mikoani pia ambapo itawafikia wakazi wa; - Arusha, Mbeya, Mwanza, Moshi na Morogoro.
Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (kulia) akikabidhi zawadi ya fulana kwa mkazi wa Chanika Abdul Wasaili (katikati) katika hafla ya kuipongeza baa ya Check point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. (Kushoto) ni mshereheshaji wa kampeni hiyo Gadner Habash.
 Mkazi wa Tabata Proper Maro (wa kwanza kulia) akipokea zawadi yake ya mfuko wenye fulana toka kwa balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi (kushoto) wakati wa wa hafla ya kuipongeza baa ya Baracuda iliyopo Tabata jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi eneo hilo mwisho wa wiki iliyopita kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wa shindano la Fanyakweli kiwanjani. (Katikati) ni Mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio E-fm Gadner Habbash.


Mpenzi wa bia ya Tusker Njau Dismas (Katikati) akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli kiwanjani Gadner Habash (kulia) mara baada ya meza yake kufikiwa na zawadi ya bia za bure na fulana katika hafla ya kuipongeza baa ya Baracuda iliyopo Tabata jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. (Kushoto) ni balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi. Nia ya kampeni hiyo ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli wanapotoa huduma kwa wateja wao.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad