JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


VALEUR YAZINDUA “VALEUR COMEDY NIGHTS” JIJINI DAR

Share This
 Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimaro akizungumza katika uzinduzi wa shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’ leo katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela Bw. Evans Bukuku
Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela, Bw. Evans Bukuku akizungumza jinsi shindano hilo litakavyofanyika katika manispaa 3 za Dar es Salaam uzinduzi huo uliofanyika wa shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’ leo katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. Na kulia ni Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimaro
Wawakilishi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) wakiongezea kuhusiana na Valeur Comedy Nights’ wakiwa na  Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela Bw. Evans Bukuku.

TANZANIA Distilleries Limited (TDL) kupitia chapa yake ya ‘Valeur Superior Brandy’, kwa kushirikiana na kampuni ya Vuvuzela Company Ltd leo hii imezindua rasmi shindano lijulikanalo kama ‘Valeur Comedy Nights’. Hili ni shindano la kusaka, kuinua na kuendeleza vipaji vya Sanaa ya ucheshi litakaloanza wiki hii jijini Dar Es Salaam.

 Vuvuzela ni kampuni inayojihusisha na Sanaa ya ucheshi, ikimiliki pia onyesho kubwa la Sanaa ya ucheshi jijini Dar Es Salaam lijulikanalo kama ‘Evans Comedy Night’.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimaro alisema. “Kauli mbiu ya chapa yetu ya Valeur Superior Brandy ni ‘Kwa story zinazonoga’. 

Watumiaji wapenzi wa Valeur hupenda sana story nzuri wakiwa katika mapumziko yao, tunaamini kwamba story nzuri na sanaa ya ucheshi vitaweza kufanya mapumziko ya wapenzi wa Valeur kuwa bora zaidi. 

Tumeungana na Vuvuzela Entertainment na tuko hapa leo kuzindua ‘Valeur Comedy Nights’. Lengo letu ni kusaka na kukuza vipaji vya Sanaa ya ucheshi hapa Tanzania, kuwafanya wasanii hawa kugundua fursa waliyo nayo kupitia sanaa hii ya ucheshi.

Bi. Warda aliendelea kusema kwamba ‘Valeur Comedy Nights’ itafanyika katika jiji la Dar Es Salaam pekee kwa sasa, lakini ina mpango wa kufika pia mikoani endapo mambo yakienda vizuri katika msimu huu wa kwanza.

 Alisema washindi 5 watakaofaulu zaidi watapata nafasi ya kujiendeleza Zaidi katika kampuni ya Vuvuzela Entertainment, na mshindi wa jumla atajipatia kitita cha shilingi 2,000,000/= taslimu. 


Aliendelea kusema kwamba wataalamu wa Vuvuzela Company Ltd ndio watahusika katika kuchuja vipaji na kusimamia shindano kwa ujumla. Bi Warda alisema pia kwamba wataalika wataalamu wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ili kusimamia mchuano uwe wa haki kwa washiriki wote.

Naye Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela Bw. Evans Bukuku alisema ‘Valeur Comedy Nights’ itafanyika kwa wiki 10 jijini Dar, ambapo kwa wiki 9 watakuwa wanasaka vipaji wilaya hadi wilaya na wiki ya kumi ni ya fainali ya mkoa kupata mshindi wa jumla.

 Aliendelea kusema usajili utafanyika siku za Alhamisi ambapo washindi 5 waliofanya vizuri watachuana katika fainali za wilaya zitakazofanyika Jumamosi hiyo. Mshindi mmoja katika kila fainali ya wilaya atapata nafasi ya kuingia katika kinyang’anyiro cha fainali za mkoa ambapo mshindi wa jumla atajipatia fedha taslimu. Bw. Evans alisisitiza kwamba kampuni yake itachukua wasanii 5 waliofanya vizuri zaidi kwa ajili ya kuwalea na kuwapa mafunzo zaidi waweze kufika mbali katika fani hii.

Bw. Evans alitaja masharti ya shindano hili kuwa ni kwa walio na umri wa miaka 18 na zaidi pekee, washiriki hawatakiwi kutoa utani juu ya mambo ya dini na siasa kwani haya hugusa hisia za watu, hawaruhusiwi kulewa wakati wa shindano nk. Alitaja pia vigezo vya ushindi kwamba ni uwezo wa kuwasilisha ujumbe katika namna ya ucheshi zaidi, uwezo wa kumiliki jukwaa vizuri, uwezo wa kuwasiliana na hadhira mbele yako nk.

Naye mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) aliipongeza sana kampuni ya TDL kupitia chapa yake ya Valeur Superior Brandy kwa kujitokeza kusaidia Sanaa hii ya ucheshi hapa Tanzania.

 Aliendelea kusema katika ulimwengu wa sasa Sanaa ya ucheshi inaweza kumfanya mtu aishi maisha mazuri sana, alitoa mifano ya mmarekani Kevin Hart na Mnigeria Basketmouth ambao wanafanya vizuri sana sasa hivi katika Sanaa hii ya ucheshi.

Alisema pia kwamba Sanaa ya ucheshi ni mpya kwa Tanzania lakini inaonyesha kukua zaidi siku za usoni na kusaidia wasanii wa Tanzania. 

Aliomba makampuni mengine yajitokeze kusaidia maeneo mbalimbali ya Sanaa ili kuwafanya vijana wengi zaidi kupata ajira katika Sanaa, pia kuwapa vijana wa Tanzania shughuli za kufanya ili wasikae vijiweni kwenye madawa ya kulevya na matatizo mengi ya dunia ya sasa.

Naye Meneja wa mauzo wa kampuni ya TDL kanda ya Dar es Salaam, Bw. Mwesige Mchuruza alielezea kwamba mashindano haya yatafanyika katika baa mbalimbali jijini Dar Es Salaam. Kwa wiki hii yakuanzia usajili utafanyika siku ya Alhamisi tar 27 July katika baa ya TCC Club Chang’ombe, na Fainali za wilaya zitafanyika siku ya Jumamosi tar 01 August katika baa hiyo hiyo na ratiba nyingine ikiwa ifutavyo;
WEEK
AUDITION OUTLET
FINAL OUTLET
LOCATION
1
TCC Club
TCC Club - Chang'ombe
Chang'ombe
2
Dar West Park
K.B Paradise - Tabata
Tabata
3
Vijana Social
Katumba Bar - Mkwajuni
Kinondoni
4
Kisuma Bar
Kisuma Bar - Mbagala
Mbagala
5
UEFA Bar
Mama Land - Ukonga
Ukonga
6
Soccer City
Mawella Bar - Sinza
Sinza
7
Brazil Pub
Brazil Pub - Tegeta
Tegeta
8
Europa Bar
Junction 98 - Buguruni
Buguruni
9
Blue Fish
Liquid Bar - Kigamboni
Kigamboni

Bi Warda alimaliza kwa kuwaalika wasanii wote wa tasnia hii ya ucheshi kujitokeza kwa wingi kuja kujisajili na kushiriki shindano hili kwani yaweza kuwa mlango wao kuelekea mafanikio makubwa ya kisanii. Aliwaalika pia wananchi wapenzi wa Valeur Superior Brand kuja kuburudika na kujionea shindano hili Jumamosi katika baa ya Tcc Club Chang’ombe jijini Dar Es Salaam. Hakuna kiingilio lakini wanaoruhusiwa ni wale tu wenye umri wa miaka 18 na zaidi.

 Wadau wa Valeur Comedy Nights na Valeur Superior Brandy.
Meneja Mkuu wa kampuni ya  Vuvuzela, Bw. Evans Bukuku akipokea hundi ya shilingi mbili kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Valeur Superior Brandy, Bi. Warda Kimar leo.
Baadhi  ya vijana wa kampuni ya  Vuvuzela wanao weza kuchekesha katika kikundi cha Comedi cha kampuni hiyo.
Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad