jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

MAMA SALMA AWASILI MALAYSIA NA KUTEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TRENI CHA SMH RAIL MJINI KUALA LUMPUR

Share This
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa watoto wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Royale Chulan iliyopo Kuala Lumpur, Mji Mkuu wa Malaysia tarehe 23.7.2015.IMG_5124
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rails Bwana Narayanan Kuppusamy mara baada ya kuwasili kwenye karakana ya treni iliyoko Kuala Lumpur nchini Malaysia Tarehe 24.7.2015.
IMG_5126
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mke wa Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rails Mama Lakshmi Narayanan ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kutembelea karakana ya treni na mabehewa huko Malaysia tarehe 24.7.2015.

 
IMG_5154
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rail Bwana Narayanan (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima kushoto) wakielekea kwenye jengo la karakana ya reli ili kujionea shughuli mbalimbali za matengenezo ya vichwa vya treni na mabehewa tarehe 24.7.2015.

IMG_5151
IMG_5149
 Mke wa Rais na Ujumbe wake wakitembelea sehemu mbalimbali zinahusika na matengenezo ya injini za treni na mabehewa.
IMG_5136
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye karakana ya SMH Rail huku Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bwana Narayanan Kuppusamy akishuhudia.
IMG_5155
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika moja ya mabehewa ya abiria yaliyokarabatiwa na kampuni ya SHM Rail na yanayotumika kubeba abiria mijini.
IMG_5163
IMG_5169
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pamoja na ujumbe wake wakipiga picha ya pamoja na mwenyeji wake Bwana Narayanan na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo mbele ya behewa lililokamilika na tayari kwa kubeba abiria.
IMG_5207
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rail Bwana Narayanan mara baada ya kutembelea karakana ya treni ya kampuni hiyo huko Kuala Lumpur Malaysia tarehe 24.7.2915.
IMG_5224
IMG_5226
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake baada ya kutembelea karakana ya injini za treni na mabehewa ya kampuni ya SHM  huko Malaysia tarehe 24.7.2015.
IMG_5231
  Mkurugenzi Mkuu wa SHM Rail Bwana Narayanan Kuppusamy akitoa neon la shukrani kwa ujio wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kutembelea karakana ya treni huko Kuala Lumpur nchini Malaysia tarehe 24.7.2015
IMG_5236
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mwenyeji wake Bwana Narayanan baada ya kumaliza shughuli ya kutembelea karakana ya treni.

Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad