Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akiizundua Kamati itakayoshughulikia
changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini kwa niaba ya Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hii imeundwa kutokana na ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino
nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto
meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi,
na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Kaimu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia jambo
wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye
Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa
alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu,
imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati
meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na
Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya
utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati
iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo
zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri
Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika
ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati
itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa
niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo
imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na
viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo
ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia
changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na
Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata
hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa
alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment