JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BENKI M YAADHIMISHA MIAKA 8 TOKA ILIPOANZISHWA

Share This
Benki M yaadhimisha miaka 8 toka ilipoanzishwa, pichani ni naibu mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jaqueline Woiso katika mkutano na waandishi wa habari wikiendi hii katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency, kuelezea mafanikio waliyopata katika kipindi hicho cha miaka 8 , kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa benki hiyo Bw. Allan Msalilwa.

BANK M Tanzania plc leo inatimiza miaka 8 toka ilipoanzishwa July 27, 2007. Akiongea na waandishi wa habari, Naibu mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema wanaadhimisha miaka minane yenye mafanikio makubwa, “mwaka 2007 tulifunga mwaka tukiwa na rasilimali zenye thamani ya TZS 32 billioni tu, na sasa tumefikia kiasi cha TZS 800 billioni. Tumekuwa tukifanya vizuri katika masoko kwa muda mrefu na tulifanikiwa kuanza kupata faida ndani ya miaka miwili (2) tu toka kuanzishwa kwa benki yetu. Kwa mwaka huu hadi kufikia June 2015 tumepata faida ya TZS 11.5 Billioni”.

 Alisema kuwa Benki hiyo ilianza na kiasi kidogo sana cha TZS 16 billioni hadi kufikia TZS 630 billioni, huku mtaji ukiwa pia umeongezeka kutoka TZS 6.5billioni hadi kufikia TZS 84 billioni kwa sasa huku idadi ya wafanyakazi pia imeongezeka kutoka 40 hadi 236, kwa uwiano wa asilimia 50% kati ya wanaume na wanawake.

Kwa upande wa huduma kwa wateja, Bi woiso alisema kuwa Benki M imekuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma masaa 12 kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku, siku 7 za wiki yaani Jumapili hadi Jumapili. “Pia tunatoa Garantii endapo tutazidisha muda tuliokubaliana kufanikisha miamala ya wateja, huduma hii inajulikana kama SSG (Service Standard Guarantee)” aliongeza.

Benki hiyo pia imekuwa ikishiriki kwa kiasi kikubwa katika kusaidia jamii ikiwa ni moja ya sera kubwa za benki hiyo ambayo huiita Money@heart, alisema Woiso. “tunashirikiana na taasisi mbalimbali katika kufanikisha miradi mingi kwenye jamii katika sekta ya Afya, Elimu, Maji Utunzaji wa mazingirana pia kuwainua wajasiriamali na wasanii wa michoro ya asili nchini”.

 Pia alisema kuwa wamefanikiwa kupata tuzo mbalimbali za kimataifa ikiwemo tuzo ya benki bora ya biashara kwa mwaka 2015 iliyotolewa katika soko la hisa la London, Benki bora katika sekta ya biashara za makampuni Afrika Mashariki na Benki bora inayoshiriki katika maendeleo ya jamii Afrika Mashariki zilitolewa na Banker Africa.

“Hatimaye tumefanikiwa kuwa chaguo bora katika benki zinazotoa huduma kwa makampuni nchini (Preffered Bank)”, alimalizia Bi Woiso.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad