JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


UZINDUZI WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA SHINYANGA

Share This
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bwana Michael Mhando akitoa taarifa fupi kuhusu mpango wa huduma ya madaktari bingwa unaoendeshwa na NHIF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bwana Alli Nassoro Rufunga akizungumza na wananchi na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga waliokuja kupata huduma kabla ya kzindua rasmi mpango huo.
 Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliokuja kupata huduma za madaktari bingwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga vifaa tiba vitakavyotumika katika zoezi hilo la siku tano.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akisalimiana na mmoja  wa madaktari bingwa Dokta Vicencia Sakware ( Mtaalamu wa Dawa za Usingizi na Wagonjwa Mahututi)
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa KItaalamu Dokta Frank Lekey baada ya uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa.
 
Akizungumza kuhusu mpango huo wa kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando amesema Mfuko unatekeleza mpango huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kupeleka huduma bora za matibabu kwa wananchi wote. 

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo unakusudia kuwapunguzia wananchi wamikoa ya pembezoni gharama za kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa ambazo ziko mbali na maeneo wanayoishi.

Hadi sasa mpango huo umeshatekelezwa katika mikoa ya Lindi, Kigoma, Rukwa, Katavi, Pwani, Tabora, Mara Manyara na Mtwara na kuwanufaisha zaidi ya wananchi 7800.
 
Katiba hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amewapongeza madaktari  bingwa hao kwa moyo wao wa kujitolea na kuwataka wengine kuiga mfano wao. Aidha amemwagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa tiba  vilivyotolewa na NHIF viendelee kutunzwa ili viwanufaishe wananchi wengi zaidi.

Bwan Rufunga pia amewahimiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujiunga  kwa wingi katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waondokane na unyonge wa kutibiwa kwa kutumiwa fedha taslimu  na badala yake watibiwe kwa kutumia kadi za CHF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad