Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo,wakati akizungumzia ushindi wake na uzoefu alioupata katika Jumba hilo la Big Brother huko nchini Afrika Kusini.Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi.
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
Idris akizungumza.
Alikuwa Mshiriki mwenza wa Idris Sultan,Irene Laveda akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akizungumza jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika katika Hoteli ya Hyatt Regency kumsikiliza Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan.
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan (pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu (pili kulia),Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) pamoja na Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a Mzee wa Mtaa kwa Mtaa
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan (pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu (pili kulia),Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) pamoja na Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a Mzee wa Mtaa kwa Mtaa
Wadau wakipiga picha ya pamoja na Idris na Laveda.
Mpiga picha na Blogger,Salma Msangi kazini.
Na Bakari Issa,Dar es Salaam
Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan ameeleza siri ya mafanikio yake katika shindano lililomalizika hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini mbele ya waandishi wa habari waliofika kumsikiliza leo kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Idris alifanikiwa kupata ushindi huo baada ya kupigiwa kura na nchi tano ambazo ni Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda pamoja na Namibia na kutwaa Dola za Kimarekani 300,000 sawa na shilingi Milioni 500 za Kitanzania na kufanikiwa kumbwaga mpinzani wake,Tayo kutoka nchini Nigeria.
Idris amesema kuwa ushindi huo ni kwa ajili ya mashabiki hususan waliompigia kura wakati akiwa katika jumba la Big Brother huko Afrika ya Kusini na kutoa shukrani kwa nguvu,bidii ambazo watu walimuekea yeye na kupata ushindi huo.
“Ushindi huu si wa kwangu peke yangu bali ni ushindi wa mashabiki ambao waliniwekea nguvu pamoja na bidii na kufanikisha ushindi huu,”alisema Idris.
Pia Idris amezitaja changamoto alizokutana nazo katika jumba la Big Brother kuwa ni kutokumjua mtu kama anakurekebisha au anakutoa kwenye njia,hivyo basi kushindwa kujua njia sahihi ya kushindana.
“Kutokujua Waafrika wanafikiriaje, hauwezi kujua mtu anakurekebisha au anakupotosha au anakutoa kwenye njia,unashindwa kufahamu hiyo ndiyo changamoto niliokutana nayo,”alieleza Idris
Aidha, amewataka washiriki wa Tanzania watakaokuja kushirika shindano hilo,wasifikirie watu wanafanya nini ndani ya jumba bali wafanye wao kama wao na sio kumuiga mtu mwingine.
hongera Sultan.Hakikisha ushindi huo unakutoa kwenye umaskini milele.Chuja marafiki,siyo muda wa kujirusha..ni muda wa kubadilisha kabisa maisha yako na familia yako
ReplyDelete