Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limeungana na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa na wahanga wa Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, maarufu kama Remembrance Day, kwa kutoa wito wa kuheshimu uhai, kudumisha amani na kuhifadhi historia ya binadamu.Katika taarifa iliyotolewa Novemba 8, 2026, jijini Dar es Salaam, TRAMEPRO imetambua umuhimu wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Mashujaa wa Vita vya Jumuiya ya Madola (Commonwealth War Cemetery), yaliyohudhuriwa na Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey, Mshauri wa Masuala ya Ulinzi, Commodore Agyapal Singh, maafisa wa Ubalozi wa India pamoja na wanajumuiya wa India wanaoishi nchini.
Shirika hilo limeipongeza Serikali ya India kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kwa kuendeleza utamaduni wa kuwakumbuka na kuwaenzi watu waliopoteza maisha yao katika vita, likieleza kuwa uwekaji wa mashada ya maua na sala ni ishara ya heshima, mshikamano na kuthamini historia ya binadamu.
TRAMEPRO imeeleza kuwa maadhimisho hayo yanatokana na historia ya kusitishwa kwa mapigano ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Novemba 11, 1918, kupitia makubaliano ya Armistice, ambapo baadaye Novemba 11 ikawa siku ya kuwakumbuka wahanga wa vita mbalimbali duniani.
Aidha, shirika hilo limeeleza kuwa Jumapili ya pili ya Novemba huadhimishwa kama Remembrance Sunday katika utamaduni wa Jumuiya ya Madola, ambapo mwaka huu imeangukia Novemba 8, 2026.
Katika kuhusisha historia hiyo na Tanzania, TRAMEPRO imekumbusha nafasi ya Tanganyika katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, wakati eneo hilo lilipokuwa likijulikana kama Afrika Mashariki ya Kijerumani, ambapo mapigano yalihusisha majeshi ya Ujerumani na Washirika, wakiwemo wanajeshi kutoka India na mataifa mengine.
Pia, shirika hilo limehimiza kutambuliwa kwa mchango na athari za vita kwa Waafrika, wakiwemo askari wa King’s African Rifles na wananchi walioguswa na mapigano hayo.
Katika hatua nyingine, TRAMEPRO imepanua wito huo wa kumbukumbu kwa kuwakumbuka pia wataalamu wa Tiba Asili na wahifadhi wa maarifa ya jadi waliotangulia mbele ya haki, ikieleza kuwa mchango wao katika kuhudumia jamii, kuhifadhi maarifa na kutumia rasilimali za asili unapaswa kuenziwa.
Limesisitiza kuwa heshima kwa wataalamu hao inapaswa kuonekana kupitia juhudi za kuendeleza utafiti, elimu, usalama wa wagonjwa, maadili ya kitaaluma na uhifadhi wa mazingira.
Katika wito wake kwa Serikali za dunia, taasisi za dini na jamii, TRAMEPRO imehimiza matumizi ya diplomasia na mazungumzo katika kutatua migogoro, kulindwa kwa maisha ya raia na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa katika kudumisha amani na haki za binadamu.
Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea kuhubiri upendo, msamaha, uvumilivu na mshikamano, huku vijana wakihimizwa kujifunza historia ili kuelewa athari za vita na umuhimu wa kujenga dunia yenye amani.
Kwa upande wa wataalamu wa afya na Tiba Asili, shirika hilo limewataka kuweka usalama wa wagonjwa mbele, kuendeleza tafiti na kuhifadhi maarifa ya jadi kwa kuzingatia maadili na haki za jamii.
Akihitimisha ujumbe huo, Katibu Mkuu wa TRAMEPRO, Boniventura F. Mwalongo, amesisitiza kuwa kumbukumbu ya mashujaa na wahanga wa vita inapaswa kuwa fundisho kwa dunia kuhusu umuhimu wa kulinda maisha, kuheshimu utu na kujenga mshikamano.
Amesema amani si kutokuwepo kwa vita pekee, bali pia ni uwepo wa haki, usalama, afya bora, upendo na mazingira salama kwa kila mwanadamu.
TRAMEPRO imehitimisha kwa ujumbe wake wa kimataifa “Lest We Forget” (Hatutasahau), huku ikisisitiza kuwa amani ni wajibu wa kila mmoja katika kujenga dunia bora kwa vizazi vijav


No comments:
Post a Comment