JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RAIS SAMIA ASISITIZA USAWA WA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Share This

Na Janeth Raphael -MichuziTv 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha huduma bora za afya ya mama na mtoto zinapatikana kwa usawa kwa wanawake na watoto wote nchini, kwa kuzingatia mahitaji yao na changamoto zinazowakabili, hususan katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa huduma za afya.

Rais Samia amesema amefurahishwa na kaulimbiu ya mkutano huo inayolenga kuharakisha matokeo yenye usawa katika huduma za afya ya mama na mtoto kupitia ugharamiaji endelevu, ubunifu katika kutatua changamoto na mifumo imara ya afya nchini Tanzania.

Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi, Novemba 26, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe, ambapo ameongeza Kuwa  kaulimbiu hiyo imebeba ujumbe muhimu unaoonesha umuhimu wa kuhakikisha huduma za afya ya mama na mtoto zinawafikia walengwa kwa kuzingatia mahitaji yao, badala ya kuwa na utofauti wa upatikanaji wa huduma kutokana na maeneo wanayoishi.

Rais Samia amebainisha kuwa upatikanaji wa huduma bora za afya ya mama na mtoto ni jambo lisilopaswa kupingwa, akisisitiza kuwa wanawake na watoto wanapaswa kupata huduma stahiki kwa wakati na kwa kuzingatia mahitaji yao ya kiafya.

Amesema maeneo yenye upungufu mkubwa wa huduma za afya yanapaswa kupewa kipaumbele katika mipango ya kuboresha huduma hizo, ili kuhakikisha wanawake na watoto wanaoishi katika maeneo hayo hawabaki nyuma katika upatikanaji wa huduma muhimu.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ugharamiaji endelevu wa huduma za afya, matumizi ya ubunifu katika kutatua changamoto zinazojitokeza pamoja na kuimarisha mifumo ya afya, akieleza kuwa hatua hizo ni muhimu katika kuharakisha matokeo yenye usawa kwa afya ya mama na mtoto.

Kauli hiyo ya Rais Samia imeweka msisitizo katika umuhimu wa kuendelea kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto nchini, kwa kuhakikisha rasilimali, mifumo na juhudi zinazowekwa zinakwenda sambamba na mahitaji ya wanawake na watoto, hasa wale wanaoishi katika maeneo yenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya.

“Niseme nimefurahishwa na kaulimbiu ya mkutano huu, isemayo:  Kuharakisha Matokeo yenye Usawa ya Huduma za Mama na Mtoto kupitia Ugharamiaji Endelevu, Ubunifu katika Kutatua Changamoto, na Mifumo Imara ya Afya nchini Tanzania. Hakika, hakuna anayeweza kupingana na ukweli huu, kwamba huduma bora za mama na mtoto zinapaswa kuwafikia wanawake na watoto kulingana na mahitaji yao, hasa katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa huduma.” Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na viongozi mbalimbali, wadau wa masuala ya Afya kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba, 2026.


Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisaini Mkataba pamoja na Wakuu wa Mikoa kuhusu usimamizi na utekelezaji wa Mkakati wa kusimamia huduma ya afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba, 2026. Kwa upande wa Wakuu wa Mikoa, Mkataba huo ulisainiwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Manyara.



Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza jambo na Mhe. Dkt. Austin Demby, Waziri wa Afya wa Sierra Leone, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba, 2026.







Viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakiwa kwenye Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba, 2026.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad