JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAKAMU WA RAIS ATOA KASI MPYA YA MAENDELEO KUSINI

Share This

 


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza ziara ya kikazi mkoani Lindi na kupokelewa kwa shangwe na mahaba makubwa, tarehe 14 Novemba 2026.

Ziara imehusisha ukaguzi wa ujenzi wa stendi ya mabasi kwenye halmashauri ya Mtama; kukagua ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kuna Chuo cha Sayansi za Kilimo na Teknolojia ya Chakula; kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Sokoine; kukagua ujenzi wa Soko la Lindi Mjini na kuongea na wananchi katika maeneo tofauti yakiwemo Mtama, Kata ya Madangwa na Lindi mjini kwa lemgo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi.

Aidha, ziara hiyo ni mwendelezo wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo ulioanza Mkoa wa Ruvuma tarehe 8 Novemba 2026 na kuendelea Mtwara, ambapo miradi ya maji, barabara, viwanda ilikaguliwa. Serikali pia ilitoa maelekezo ya kulipwa kwa wakati madeni ya wakulima wa Tumbaku na kusisitiza upatikanaji wa pembejeo muhimu, ikiwemo salfa, ili kuongeza tija na ushindani wa zao la Korosho katika msimu ujao wa Kilimo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), ameahidi kuhakikisha ugawaji wa salfa kwa wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara unaanza mwezi Machi 2027, hatua inayolenga kuimarisha uzalishaji, kuongeza kipato cha wakulima na kuchochea ukuaji wa uchumi wa maeneo hayo.

Kwa msisitizo, Makamu wa Rais amewasihi viongozi kutatua changamoto za wananchi na kuleta matokeo yanayoonekana, kwani wananchi wanahitaji kuona utekelezaji na mafanikio ya vitendo.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad